Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Issa Ali Abbas Mangungu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbagala

Primary Question

MHE. ISSA A. MANGUNGU aliuliza:- (i) Je, ni lini ujenzi wa kituo kidogo cha kupoza umeme (substation) ya Mbagala utakamilika? (ii) Je, makubaliano ya mkataba wa ujenzi wa kituo hicho ulikuwa wa muda gani? (iii) Je, mkandarasi wa mradi huo yupo ndani ya muda au amechelewesha kazi kwa mujibu wa mkataba na je ni hatua gani zimechukuliwa?

Supplementary Question 1

MHE. ISSA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa fursa ya kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza. Kwanza nampongeza Mheshimiwa Waziri na Mheshimiwa Naibu Waziri kwa ushirikiano walioutoa kwa wananchi wa Mbagala mpaka mradi huu kukamilika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa kuwa baada ya kukamilika substation ya Mbagala, Mbagala ni eneo ambalo lina viwanda; je, wana mkakati gani sasa kuvishawishi viwanda vilivyopo Mbagala kutumia gesi asilia ili kupunguza low voltage ambayo tunaipata kutokana na matumizi ya viwanda vile?
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini Serikali itafanya eneo la Mbagala (District) kuwa Mkoa kwa sababu ina wateja wengi na TANESCO imeelemewa kule Mbagala kiasi kwamba inashindwa kupaleka umeme katika maeneo ya Toangoma, Vigozi, Mponda na maeneo mengine?

Name

Subira Khamis Mgalu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri tumepokea pongezi zake, nasi kwa kweli tunamshukuru sana kwa ushirikiano alioufanya kwa kipindi chote cha utekelezaji wa mradi huu Jimboni kwake Mbagala.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge ameeleza mkakati wa Serikali wa kuvishawishi viwanda kutumia gesi asilia. Naomba nimthibitishie Mheshimiwa Mbunge Wizara yetu kupitia TPDC tuna mkakati wa kusambaza gesi asilia kwa matumizi ya viwanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata kwa mwaka huu wa fedha ambao utaanza 2018/2019 TPDC imeshaingia makubaliano ya awali ya kusambaza gesi katika maeneo mbalimbali ya viwanda yaliyopo Mkuranga, kwa mfano Kiwanda cha Bakhressa, Loth Steel cha Mkuranga na pia hata Kiwanda cha Biku na Cocacola Kwanza, Dar es Salaam.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, wazo lake hilo linafanyiwa kazi na viwanda tunavihamasisha vitumie gesi kwa sababu gesi ipo na ya kutosha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, ameuliza ni lini tutaifanya Mbagala kuwa Mkoa? Naomba nilichukue hili suala na linajadilika ndani ya Wizara, tunaweza tukalifanyia kazi. Ni kweli Mbagala ina wateja na watumiaji wengi wa umeme. Naomba hili tulichukue. Ahsante. (Makofi)