Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jaku Hashim Ayoub

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. JAKU HASHIM AYOUB aliuliza:- Mawaziri kama walivyo viongozi wengine wa Serikali, wapo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi na kwamba wananchi wamewachagua Wabunge na Mawaziri (Serikali) ili kuwasiliana, kushirikiana na kushauriana katika kutatua kero zao; lakini kwa bahati mbaya sana wapo baadhi ya Mawaziri ambao kupatikana kwao hata kwenye simu ni jambo gumu kupita kiasi:- a) Je, Serikali haioni kuwa ipo haja ya Mawaziri wenye tabia hiyo ya kujichimbia na kutopatikana kwenye simu kuacha tabia hiyo kwa maslahi ya wananchi? b) Je, Serikali itakubaliana nami kuwa ipo haja ya kuweka utaratibu maalum wa kuifikia Serikali iwapo wananchi kupitia Mbunge wao wana shida ya kumuona Waziri anayehusika na akawa hapatikani hata kwa simu?

Supplementary Question 1

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri kutokuwa na afya kwa upande wangu, niwapongeze sana Naibu Mawaziri; Mheshimiwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mheshimiwa Engineer Atashasta Nditiye na Naibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji, kwa kupokea simu kwa wakati, niwapongeze sana kwa hili na wengine naomba wafuate mfano huu.
Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, hizo Kanuni nani anazisimamia ili hao Mawaziri ambao wamo humu ndani, hawapokei simu zikiwemo za Wabunge, mbali na za wananchi, ili hatua zichukuliwe? Ikiwa namba za ma- RPC ziko hadharani na ziko katika mtandao, sababu gani zinazosababisha Mawaziri hao namba zao zisiwe hadharani? Hilo la kwanza.
Mheshimiwa Spika, la pili, Mheshimiwa Waziri kabla ya kupata Uwaziri hapa, Mheshimiwa Spika ni shahidi, alikuwa mkali kutetea wananchi wake na akawa ngangari kwelikweli. Ni lini Mawaziri namba zao zitatangazwa hadharani ili wananchi na Wabunge watakapowapigia simu wapokee?

Name

Capt. (Mst). George Huruma Mkuchika

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Newala Mjini

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA): Mheshimiwa Spika, maswali yake kwa kweli ni moja lilelile limejirudia lakini pia nafikiri kuna mchanganyiko kidogo katika swali lake. Analalamika kwamba Mawaziri hawapatikani kwa simu lakini wakati huohuo analalamika kwamba namba zao haziko hadharani. Sasa hao ambao huwapati kwa simu ni wapi kama simu zao hunazo? (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Spika, sasa kwa kujibu swali lake, nani anazisimamia hizo Kanuni nilizozitaja? Kanuni zinasimamiwa na Serikali, kila Wizara kuna viongozi wake na Wizara ya Utumishi inasimamia Kanuni zote za watumishi wa umma.
Mheshimiwa Spika, sasa ilimradi tumeshasema katika jibu la msingi kwamba hatuna ushahidi wa Waziri ambaye kwa makusudi hataki kupatikana, ndiyo maana hatujamchukulia hatua maana hatuna taarifa hizo. Kila Waziri hapa ana mkubwa juu yake, akizileta kama mimi siyo size yangu nitazipeleka juu, lakini atuletee na siyo kwako wewe tu, Mtanzania yeyote yule ambaye anaona kwamba hakutendewa haki, hampati Waziri kwa makusudi, hilo kwa makusudi naliweka kwenye, Wazungu wanasema inverted commas, maana yake mimi sina ushahidi nalo hilo.
Mheshimiwa Spika, ndiyo maana kila Wizara kuna sanduku la maoni. Sanduku lile una jambo la kuishauri Wizara, una jambo umetendewa vizuri na Wizara unaandika unawapongeza, una jambo umefanyiwa vibaya na Wizara unaandika unawasema.