Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ajali Rashid Akibar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Newala Vijijini
Primary Question
MHE. MHE. AJALI R. AKBAR aliuliza:- Madini aina ya Coltan yamegundulika katika Wilaya za Ruangwa, Masasi na Newala, lakini Wizara ya Madini imeweka beacon katika Kijiji cha Nandimba, Kata ya Chilagala. (a) Je, ni utaratibu gani umetumika kuweka beacon katika Wilaya nyingine? (b) Je, Serikali haioni kupora rasilimali ya wilaya nyingine kunaweza kusababisha migogoro? (c) Je, ni lini Serikali itamaliza mgogoro huo?
Supplementary Question 1
MHE. MHE. AJALI R. AKBAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri; lakini naomba nimuulize maswali mawili madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, Wilaya ya Newala na Masasi hatuna mgogoro wa kimpaka ila migogoro ya mipaka watasababaisha watu wa madini. Kitendo cha viongozi wa Wilaya nyingine kwenda kufanya tathmini na kusema wao watalipa fidia kwenye wilaya nyingine wakati viongozi wapo kinavunja heshima kwa viongozi wa wilaya nyingine. Kwa hiyo inaonekana kabisda kwamba viongozi wa wilaya nyingine hawafanyi kazi. Je, Serikali ipo tayari kuacha kuwadhalilisha viongozi wa Wilaya ya Newala kuonekana hawafanyikazi na wanaofanyakazi ni Wilaya ya Masasi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, itakapotokea mrabaha, kama hawa wananchi wa Newala wanakwenda kufanyiwa tathmini Masasi italipwaje na Wilaya ya Newala itapataje haki zake? Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Name
Stanslaus Haroon Nyongo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Maswa Mashariki
Answer
NAIBU WAZIRI WA MADINI (MHE. STANSLAUS H. NYONGO): Mheshimiwa Mwenyekiti, mgogoro kati ya wilaya moja hadi nyingine, kwa maana ya mgogoro wa viongozi, nadhani ni kwamba ni vizuri tu viongozi hao wakakaa chini wakaelewana kwa sababu hakuna haja ya kugombana katika hatua hii wakati Kampuni ya Natural Resources inafanya utafiti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kuhusu mrabaha; hatua za utafiti ni hatua za mwanzo za uchimbaji. Pale madini yatakapogundulika kwamba Kampuni hii imefanya utafiti ikagundua madini yaani katika wilaya zote mbili kwa maana ya Newala na Masasi, basi sisi kama Wizara tutakaa chini na tutaangalia namna ya halmashauri hizi mbili kuweza kuneemeka katika kupata service levy na wala si mrabaha kwa sababu mrabaha wenyewe unakusanywa na Wizara moja kwa moja, kwa hiyo hakutakuwa na ugomvi, lakini katika service levy kwa sababu ni ushuru ambao unakwenda katika halmashauri, tutaangalia na tutakaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hilo siyo suala jipya, kuna maeneo mengine unakuta halmashauri mbili zinaweza zikaneemeka katika service levy kwa maana katika mradi mmoja. Kwa hiyo tutaangalia namna ya service levy zitakavyogawanywa kwenda katika wilaya hizo mbili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile, utafiti utakapokwisha tutajua kwa sababu inawezekana ile leseni ya utafiti iko wilaya mbili lakini baadaye utafiti ukaonesha kwamba madini haya yapo wilaya moja, kwa hiyo wilaya hiyo ndiyo itakayoneemeka na ushuru wa service levy. Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved