Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Sikudhani Yasini Chikambo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SIKUDHANI Y. CHIKAMBO aliuliza:- Baadhi ya Mahakama za Mwanzo kama vile Matemanga, Napakanya na nyingine nyingi ni chakavu na hazipati fedha kwa ajili ya ukarabati hali inayosababisha Mahakimu na watumishi wengine kufanya kazi katika mazingira magumu sana:- Je, ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa Mahakama hizo?
Supplementary Question 1
MHE. SIKUDHANI Y. CHIKAMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Sisi sote tunafahamu kwamba mahakama ni chombo cha kisheria ambacho kimekuwa kikitoa haki na kuleta amani katika maeneo mbalimbali kwa mujibu wa sheria. Je, Serikali haioni kuchelewa kuweka mazingira mazuri ya kufanyia kazi kwa watumishi wa mahakama wakiwemo Mahakimu ni kudhoofisha hali ya utendaji kazi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika jibu la Mheshimiwa Waziri la msingi amekiri kama mahakama hizo ni chakavu na majengo mengi ni yale yaliyoachwa na Mkoloni, je, ni nini tamko la Serikali la kuharakisha ujenzi wa mahakama hizo sambamba na ujenzi wa nyumba za Mahakimu? Ahsante.
Name
Anthony Peter Mavunde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Dodoma mjini
Answer
NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA):
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Serikali inatambua changamoto iliyokuwepo katika ujenzi wa mahakama na kwa muda wote tumeendelea kutenga fedha kwenye bajeti zetu kuhakikisha kwamba tunakabiliana na changamoto hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mpango wa Wizara tumeamua kushirikiana na Baraza la Nyumba la Taifa na Chuo Kikuu cha Ardhi ili kupitia ujenzi wa nyumba za mahakama na ofisi za mahakama kwa kupitia teknolojia mpya ya moladi tuweze kuzifikia mahakama nyingi zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimwondoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba ni mpango wa Serikali wa kuhakikisha kwamba tunajenga mahakama nyingi kadri iwezekanavyo na hii itatokana na upatikanaji wa fedha. Uzuri tunayo teknolojia mpya ya moladi, naamini tutawafikia wananchi wa Tunduru na wao wapate huduma hii ya mahakama. Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved