Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kiswaga Boniventura Destery

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Magu

Primary Question

MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA aliuliza:- Serikali inaanzia katika ngazi ya kitongoji, mtaa na kijiji:- Je, ni lini viongozi na Wenyeviti wa Vitongoji, Mtaa na Kijiji watalipwa mishahara?

Supplementary Question 1

MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa hata sisi viongozi wa Bunge mojawapo ya sifa ni kuwa na kazi halali zinazotuingizia kipato kama hawa Wenyeviti wa Vitongoji ambao sisi tunalipwa, wao hawalipwi. Je, Serikali iko tayari kuleta sheria ili waweze kulipwa mishahara? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa viongozi hawa ndiyo wanaohamasisha maendeleo kama ujenzi wa zahanati, shule za msingi, sensa na kusimamia amani, je, Serikali iko tayari iko tayari kuendelea kuwalipa posho? (Makofi)

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la kwanza, napenda nimhakikishie kwamba wakati wowote Serikali inapopata mapendekezo huwa inayafanyia kazi. Kwa hiyo, mara tutakapopata mapendekezo kutoka kwenye vikao halali vinavyohusika tunaweza wakati wowote tukafanya marekebisho ya sheria kutokana na muktadha wa muda utakavyokuwa na mapendekezo yatakavyokuwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili kuhusu kulipa posho, Serikali ilishatoa Mwongozo tangu mwaka 2003 kwamba yatumike mapato ya ndani kulipa posho kwa viongozi hawa na posho zile zimeainishwa. Kwa hiyo, ni jukumu la Wakurugenzi wa Halmashauri na Mheshimiwa Mbunge namwomba sana asimamie kwenye jimbo lake na watumie Mwongozo huo kuhakikisha kwamba viongozi wetu hawa wanalipwa posho.