Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Hamida Mohamedi Abdallah
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Lindi Mjini
Primary Question
MHE. HAMIDA M. ABDALLAH (K.n.y MHE. IBRAHIM HASSANALI MOHAMMEDALI) aliuliza:- Wananchi au taasisi zilizopewa vibali vya kupaki magari hadi saa 12 jioni katika Jiji la Dar es Salaam sasa wanatumia vibali hivyo kupaki kwa saa 24. Hali hiyo imeibua usumbufu kwa wananchi wanaotaka kupaki magari yao kuanzia saa 12 jioni:- Je, ni lini Serikali itakomesha suala hilo ili kuwaondolea wananchi usumbufu wanaoupata?
Supplementary Question 1
MHE. HAMIDA M. ABDALLAH: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa majibu mazuri ya Serikali lakini napenda kuuliza swali la nyongeza, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, hiki kimekuwa ni chanzo kizuri cha mapato katika maeneo ya majiji, manispaa na maeneo mbalimbali nchini. Hata hivyo, kumekuwa na kero kubwa sana kwa sababu ya kutosimamiwa vizuri kwa sheria hii. Pamoja na kwamba Mheshimiwa Waziri amewatangazia Wakurugenzi wa Halmashauri pia wangepelekewa maagizo haya kwa maandishi ili sheria hii iweze kusimamiwa na kupunguza kero ambayo ipo sasa hivi. Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba nijibu na nipokee ushauri wa kutoka kwa Mheshimiwa Hamida na nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maelezo yake anasema kwamba chanzo hiki pamoja na kwamba ni cha uhakika lakini kimekuwa kero na mimi naomba niungane naye. Katika maeneo mengi unakuta kwamba mtumiaji anapo-park inakuwa kama ni suala la kuviziana, kwamba je, huyu atakosea ili adhabu iweze kutolewa. Naomba niwaagize Wakurugenzi wote kusimamia sheria hii lakini pia alama za parking ziwe ni zile ambazo zinaonekana kwa kila mtu ambaye anatumia gari ili anapo-park isije ikaonekana kwamba ni wrong parking.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved