Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Venance Methusalah Mwamoto
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilolo
Primary Question
MHE. VENANCE M. MWAMOTO (K.n.y MHE. HALIMA A. BULEMBO) aliuliza:- Kagera ni moja ya mikoa mitano maskini zaidi nchini kutokana na utafiti uliofanywa na Bwana Joachim De Weeidt na kuchapishwa kwenye jarida la Journal of Development Studies ambao unaonyesha kuwa kuna njia mbili za kuondoa umaskini Kagera ambazo ni kilimo na biashara:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwa na miradi maalum ya kuondoa umaskini kwa watu wa Kagera ambao ndiyo mkoa pekee unaopakana na nchi nyingi zaidi za EAC na hivyo kuufanya kuwa Mkoa wa kimkakati kibiashara?
Supplementary Question 1
MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na jibu zuri la Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba niulize maswali madogo ya nyongeza, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza, kwa kuwa Mkakati wa East African Community ni kuhakikisha wanaondoa umaskini si kwa Kagera tu bali na mikoa mingine. Tatizo kubwa la Mkoa wa Kagera pamoja na kuwa na viwanda vingi ni barabara zao kutopitika kwa muda mrefu na kusababisha viwanda vyao visifikiwe kwa wakati na kusafirisha mali nje. Je, Serikali ina mkakati gani?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa kuna baadhi ya mikoa ambayo pia imekuwa ina tatizo ambalo linafanana ikiwepo Mkoa wa Iringa tuna uwanja wa ndege, pamoja na kuwa kuna mazao mengi ambayo yanatoka na yanafika nchi za Afrika Mashariki lakini Serikali imekuwa ikisuasua katika ujenzi wa uwanja ule.
Ni lini sasa Serikali itahakikisha kwamba ule uwanja wa ndege unamalizika ili tupate na watalii wa kutosha waweze kwenda Ruaha National Park kwenye Jimbo la Ismani?
Name
Eng. Atashasta Justus Nditiye
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muhambwe
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambako maswali ya Mheshimiwa Mwamoto yamelenga, naomba kuyajibu maswali yake mawili, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ni kweli kwamba hapo katikati kulikuwa na changamoto ya barabara, baadhi ya barabara kwa kweli zimekuwa na hali mbaya lakini Serikali imekwishapeleka fedha na kuna tangazo la kutafuta wakandarasi kwa ajili ya kurekebisha barabara za Bukoba na maeneo mengine mbalimbali ya nchi yetu ili ziweze kupitika kupeleka mazao sehemu mbalimbali.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la pili, tumekwisha tangaza tenda na kuna mkandarasi ambaye yuko tayari kwenye Uwanja wa Ndege wa Iringa, tunasubiri taratibu za mwisho za kuwalipa ili waweze kufanya ukarabati unaostahili. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved