Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Allan Joseph Kiula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Iramba Mashariki
Primary Question
MHE. ALLAN J. KIULA aliuliza:- Wakazi wa Jimbo la Mkalama wanapata shida sana kufuata huduma za Mahakama katika Wilaya ya Iramba – Kiomboi, umbali mrefu kutoka Mkalama:- (a) Je, ni lini Serikali itajenga Mahakama ya Wilaya yalipo Makao Makuu ya Wilaya ya Mkalama? (b) Je, Serikali ipo tayari kuanzisha Mahakama ya muda ya Wilaya katika majengo ya Mahakama ya Mwanzo Nduguti?
Supplementary Question 1
MHE. ALLAN J. KIULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Kwanza niipongeze Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuweza kujenga hiyo Mahakama ya Mwanzo, ni Mahakama nzuri na ya kisasa. Swali la nyongeza, kwa kuwa, Mheshimiwa Waziri amesema Mahakama ya muda itaanza kabla ya mwisho wa mwezi Juni. Je, ni lini maandalizi ya kuhamisha mafaili ya kesi zilizopo Kiomboi kwenda Iguguno yataanza ili wakati wa uzinduzi na mafaili yawepo? Tusije tukapeleka wafanyakazi halafu kukawa hamna mashauri ya kusikiliza?
Name
Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilosa
Answer
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Kiula, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeyapokea mapendekezo yake ya kuhakikisha kuwa kabla ya mwezi Juni, 2019 mafaili yawe yamehama kutoka Mahakama ya Kiomboi kwenda Iguguno. Nami nimhakikishie kuwa, ushauri huo tumeuchukua, tutaufanyia kazi na tutahakikisha kabla ya tarehe hiyo, mafaili hayo yatakuwa yamekwishahamia katika Mahakama ambayo imepangwa.
Name
Abdallah Majurah Bulembo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nominated
Primary Question
MHE. ALLAN J. KIULA aliuliza:- Wakazi wa Jimbo la Mkalama wanapata shida sana kufuata huduma za Mahakama katika Wilaya ya Iramba – Kiomboi, umbali mrefu kutoka Mkalama:- (a) Je, ni lini Serikali itajenga Mahakama ya Wilaya yalipo Makao Makuu ya Wilaya ya Mkalama? (b) Je, Serikali ipo tayari kuanzisha Mahakama ya muda ya Wilaya katika majengo ya Mahakama ya Mwanzo Nduguti?
Supplementary Question 2
MHE. ALHAJI ABDALLAH M. BULEMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Wilaya ya Misenyi katika Mkoa wa Kagera ni wilaya iliyoanza mwaka 2007 mpaka leo ina miaka 11, lakini haina Mahakama ya Wilaya. Wilaya ile ni ya mpakani, kuna wahamiaji haramu, kuna nyarubanja kahawa, kuna matatizo mengi sana. Sasa nataka kuiuliza Serikali yangu, ni lini wilaya hii itapata haki ya kuwa na Mahakama ya Wilaya ili kuwapunguzia adha wananchi?
Name
Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilosa
Answer
WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza ya Mheshimiwa Alhaji Bulembo, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatambua kabisa kwamba, Wilaya ya Misenyi inayo mashauri mengi hasa yanayohusu masuala ya ardhi na mimi mwenyewe binafsi mwaka jana nilitembelea Wilaya ya Misenyi na nilifika na kuoneshwa eneo ambalo limetengwa ili kujenga Mahakama ya Wilaya ya Misenyi. Kwa hiyo, niahidi kwamba, tulikuwa tumepanga kuanza kujenga Mahakama ya Wilaya ya Misenyi mwaka 2017/2018, tunabadilisha mipango ili tuweze kuiwezesha Mahakama hiyo kuanza kujengwa mapema iwezekanavyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwombe Mheshimiwa Mbunge avute subira wakati wa bajeti tunaweza kuwa na maelezo mazuri zaidi ni lini ujenzi wa Mahakama ya Misenyi utaanza na kama nilivyosema mimi mwenyewe nimefika na kweli Misenyi kuna mashauri mengi sana ya ardhi.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved