Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:- Hali ya sekta ya kilimo na mifugo katika Jimbo la Same Mashariki ni mbaya licha ya kuwepo wafanyakazi wa Serikali wanaosimamia sekta hizo kwenye Wilaya, Kata na hata Vijiji. Wengi wa wafanyakazi hao wanatumia muda mwingi kufanya kazi zao binafsi badala ya kuwasaidia wakulima na wafugaji kuleta mabadiliko katika sekta hizo. (a) Je, Serikali inatumia kigezo gani kutathmini utendaji kazi wa waajiriwa hao kupima ufanisi wao? (b) Je, Serikali ipo tayari kupunguza idadi ya waajiriwa hao waliopo vijijini ili fedha itakayookolewa kutoka katika mishahara yao isaidie kutengeneza miundombinu ya umwagiliaji na malambo?

Supplementary Question 1

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda niseme tu kwamba kwa kuwa Serikali imeonekana inapeleka pesa kidogo sana ya maendeleo kwenye sekta hii ya kilimo hasa katika jimbo langu na kwa hiyo Maafisa Ugani wanakuwa wanakosa kazi za kufanya. Je, Serikali haioni ni kupoteza hela za Serikali kama watazidi kuongeza waajiriwa wakati hawana kazi za kufanya?
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili; ni wazi kwamba Maafisa Ugani hawa wanaopelekwa kwenye vijiji hawajawahi kufanyiwa semina, wengine wana miaka kumi, wala orientation ya kwamba kazi ambazo wanatakiwa wazifanye kwa kipindi hiki ni nini na kwa kuwa ukijua kwamba kozi wanazochukua haziko specific kwenye mazao yale, mtu ametoka kulima korosho leo anapelekwa kwenye ndizi, hajui hata kutengeneza migomba.
Je, Serikali haioni kwamba haijawatendea haki maafisa ugani hawa wanaopelekwa vijijini bila kufanyiwa semina na orientation za kuwafanya waelewe kile wanachotakiwa kufanya katika vijiji au kata zile pamoja na kwamba pia hawana vitendea kazi?

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la kwanza amesema kwamba Serikali inapeleka bajeti ndogo, nimwambie tu kwamba bajeti inayopelekwa na Serikali Kuu katika Halmashauri ni sehemu ndogo tu ya bajeti ya jumla ambayo Halmashauri inatakiwa ifanyie kazi. Maana yake kule kuna bajeti ya ndani inaitwa own source budget. Kwa hiyo hakuna sababu yoyote inayokubalika inayomfanya Afisa Ugani yeyote aseme kwamba ameshindwa kwenda kijijini eti kwa sababu ya bajeti ndogo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la pili amesema kwamba kuna Maafisa Ugani wamepelekwa kule lakini hawana ujuzi na mazao husika. Sisi Serikali tunachokifanya tunapeleka Afisa Ugani ambaye amesomea Sekta ya Kilimo, Sekta ya Mifugo kwenda kufanya kazi za ugani katika Halmashauri fulani, sasa akikuta kule kuna zao fulani mahususi ni kazi yake kujiridhisha kupitia tena, kudurusu documents mbalimbali zinazohusu zao hilo mahususi ili awe vizuri kitaaluma na kiuendeshaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nakubaliana naye kwamba mtu ambaye amesoma general agriculture akienda kwenye zao la tumbaku specific atalazimika kukosa baadhi ya utaalam katika zao lile, ni kweli, lakini tunawahimiza kwamba lazima wahakikishe kwamba wanalifahamu hilo zao vizuri na waweze kuwashauri wakulima vizuri kwa sababu wao ni wataalam wa kilimo. Kama mimi ni mchumi lakini nilisoma shule ya kilimo nakumbuka masomo ya kilimo wakati ule, je mtu ambaye amesoma cheti au diploma au ana degree ya kilimo, lazima atakuwa anajua vizuri zaidi. Ahsante sana.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO (MHE. DKT. MARY M. MWANJELWA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi hii niweze pia na mimi kujibu swali la mama yangu, Mheshimiwa Kaboyoka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri sana ya Naibu Waziri kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba na mimi niongezee hapo kidogo kwamba sisi kama Wizara ya Kilimo kupitia vyuo vyetu vyote vya mafunzo nchini, swali ambalo na mimi niliweza kulijibu jana, ni kwamba tumefanya mpango mkakati hata wale Maafisa Ugani ambao pia bado hawatoshelezi na tumesema wasikae ofisini, lakini tuna mpango mkakati kama Wizara ya Kilimo kuhakikisha kwamba tunawajengea uwezo hata wale ambao Maafisa Ugani wako maofisini ili waweze kutoa mafunzo kwa wakulima kuendana na mazao ambayo yapo katika hayo maeneo. Naomba kuwasilisha.

Name

Mariamu Nassoro Kisangi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:- Hali ya sekta ya kilimo na mifugo katika Jimbo la Same Mashariki ni mbaya licha ya kuwepo wafanyakazi wa Serikali wanaosimamia sekta hizo kwenye Wilaya, Kata na hata Vijiji. Wengi wa wafanyakazi hao wanatumia muda mwingi kufanya kazi zao binafsi badala ya kuwasaidia wakulima na wafugaji kuleta mabadiliko katika sekta hizo. (a) Je, Serikali inatumia kigezo gani kutathmini utendaji kazi wa waajiriwa hao kupima ufanisi wao? (b) Je, Serikali ipo tayari kupunguza idadi ya waajiriwa hao waliopo vijijini ili fedha itakayookolewa kutoka katika mishahara yao isaidie kutengeneza miundombinu ya umwagiliaji na malambo?

Supplementary Question 2

MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa matatizo ya ukosefu wa Maafisa Ugani inawakumba wananchi wa Jimbo la Ukonga katika Wilaya ya Ilala katika kata za Kitunda, Vigewe, Majowe na Mzinga. Wananchi wa eneo hilo ni wakulima wa mbogamboga na matunda lakini kuna Afisa Ugani mmoja anahudumia kata tatu, je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza Maafisa Ugani katika Jimbo la Ukonga na Wilaya ya Ilala kwa ujumla?

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba kuna upungufu wa Maafisa Ugani nchini, na kama nilivyojibu kwenye swali la msingi ni kwamba kwa maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi tunahitaji kuongeza Maafisa Ugani ambapo tukiwafikia hawa ambao tumepanga kuwaongeza kupitia maelekezo ya Ilani tunaamini tutakuwa na Maafisa Ugani wa kutosha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa Serikali ina kibali cha kuajiri watumishi takribani 52,000 na mpaka sasa hivi hatujafikia hata 20,000 katika kuajiri, kibali ambacho kitatoka hivi karibuni labda mwezi wa pili au wa tatu, tutaajiri Maafisa Ugani wa kutosha kupunguza tatizo lililopo. Naamini tutakapoajiri hao kabla ya mwezi wa sita na kata hizo ambazo umezitaja tutazipatia Maafisa Ugani. Ahsante sana.

Name

Joseph Roman Selasini

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Rombo

Primary Question

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza:- Hali ya sekta ya kilimo na mifugo katika Jimbo la Same Mashariki ni mbaya licha ya kuwepo wafanyakazi wa Serikali wanaosimamia sekta hizo kwenye Wilaya, Kata na hata Vijiji. Wengi wa wafanyakazi hao wanatumia muda mwingi kufanya kazi zao binafsi badala ya kuwasaidia wakulima na wafugaji kuleta mabadiliko katika sekta hizo. (a) Je, Serikali inatumia kigezo gani kutathmini utendaji kazi wa waajiriwa hao kupima ufanisi wao? (b) Je, Serikali ipo tayari kupunguza idadi ya waajiriwa hao waliopo vijijini ili fedha itakayookolewa kutoka katika mishahara yao isaidie kutengeneza miundombinu ya umwagiliaji na malambo?

Supplementary Question 3

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mara nyingi tukizungumza Maafisa Ugani tunazungumza zaidi habari ya maafisa hawa wa kilimo, lakini kuna wanaohusika na uvuvi, kuna wanaohusika na ufugaji na ni dhahiri kwamba upungufu ni mkubwa.
Sasa swali langu ni hili, kuna maeneo kama Jimbo langu la Rombo vijana ambao wamesoma kwenye vyuo vya kilimo, vyuo vya uvuvi na vyuo vya ufugaji wanajitolea kusaidia wakulima au wastaafu wanajitolea kuwasaidia wakulima na wanatumika vizuri sana. Je, Serikali iko tayari kuwatambua hawa na kuwasaidia ili waendelee kuwasaidia wakulima wakati utaratibu wa kuongeza watumishi wengine ukiendelea kufanyika?

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, dhana ya kujitolea au volunteering kwa Tanzania na vijana wetu na wengine wastaafu, kwa wastaafu kidogo naona inatia matumaini lakini kwa vijana ambao wamemaliza vyuo bado haijaingia vizuri katika fikra zao.
Mimi nadhani katika nchi kama India huwezi kupata ajira kabla kwanza hujapata uzoefu kupitia hata kujitolea, kwa hiyo tunahamasisha sana pale ambapo wapo wataalam wetu ambao wanaweza wakajitolea kwenye kijiji, Halmashauri ifikirie namna ya kuwaratibu na kuwapatia posho kidogo ili waweze kufanya kazi zao vizuri sana. (Makofi)