Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joseph Roman Selasini

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Rombo

Primary Question

MHE. JOSEPH R. SELASINI (K.n.y. MHE. JESCA D. KISHOA) aliuliza:- Kwa muda mrefu sasa Mkuu wa Wilaya ya Ikingu amekuwa akijichukulia sheria mkononi na kuwanyanyasa wananchi wa Kata za Ighombwe, Iglansoni na maeneo ya Wilaya ya Ikungi. Je, Serikali inaweza kutoa majibu ni mamlaka yapi aliyonayo Mkuu huyo wa Wilaya ya kuwanyanyasa na kuamrisha mali za wananchi kuchomwa moto au kuporwa na Serikali bila utaratibu wowote wa kisheria kwa kisingizio kuwa wanaishi maeneo yasiyoidhinishwa kwa makazi?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Pamoja na hayo, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, wananchi wanajenga katika maeneo mbalimbali ambayo Serikali inasema hayaruhusiwi kwa sababu ya uhaba wa ardhi lakini wakati huohuo maeneo hayo yana viongozi na baada ya kujenga wanapelekewa maji, umeme na kadhalika. Nataka kujua, Serikali inawachukulia hatua gani watendaji au viongozi wa maeneo kama hayo ambao wanawaacha wananchi wanajenga wakishakamilisha ndiyo wanaingia kwenda kuwaondoa na kwa sababu hiyo kuharibu mali zao?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, suala la kuchukua madaraka vibaya kwa baadhi ya Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa bado linaendelea nchini. Natambua juhudi za Waziri wa Nchi, Mheshimiwa Jafo na Waziri Mheshimiwa George Mkuchika na hatua mbalimbali ambazo baadhi ya Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa wamechukuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kuna wilaya nyingine kwa mfano Wilaya ya Hai, Mkuu wa Wilaya bado anaendelea na vitendo vya kuwakamata hovyo wawekezaji, wananchi na kushinikiza baadhi ya wanasiasa kwa kutumia vikosi vya askari wahame kwenye vyama vyao, hata Mkuu wa Mkoa wa Iringa…

MWENYEKITI: Uliza swali Mheshimiwa.

MHE. JOSEPH R. SELASINI: Tulikuwa naye kwenye kikao juzi hapa tukamwambia ajirekebishe, akatoka akaenda ku- tweet kwamba sasa atakwenda speed kilometa 120 badala ya 80 alizokuwa anaenda nazo, sasa hii ni insubordination kwa Serikali. Baada ya matamko yote ya Mawaziri, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa ambao bado wanaendelea ku-insubordinate Serikali ni hatua zipi ambazo Serikali imepanga kuchukua?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nimshukuru Mjumbe wa Kamati yangu ya TAMISEMI, kaka yangu Mheshimiwa Selasini kwa maswali yake mawili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza tumeshatoa maelekezo mbalimbali; jambo la kwanza watu wasivamie maeneo ambayo siyo halali kwa ujenzi, lakini jambo la pili tumetoa maelekezo kwa viongozi wetu kwa sababu wao tumewapa dhamana wahakikishe wanasimamia maeneo hayo. Kitendo cha wananchi hata kujenga sehemu isiyoruhusiwa halafu tunawaangalia mwisho wa siku kuja kuwabomolea sio jambo sawasawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, maelekezo hayo tumeshayatoa. Ndiyo maana Mheshimiwa Rais ametoa maelekezo katika baadhi ya vijiji na kuna Kamati Maalum inaongozwa na ndugu yangu Mheshimiwa Lukuvi inafanya kazi hiyohiyo lakini na maelekezo mengine ya Kiserikali tunayafanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini swali la pili la kwamba baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wanaendelea kufanya mambo ambayo siyo sawasawa, ni kweli Mheshimiwa Mbunge unafahamu kwamba tulipotoka hali ilikuwa ni mbaya sana. Tulikuwa na idadi kubwa sana ya Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya hali kadhalika Wakurugenzi wa Halmashauri, hasahasa Wakuu wa Wilaya walikuwa wakifanya mambo sivyo lakini kazi kubwa iliendelea kufanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi ndani tunafanya tathmini hali imebadilika sana lakini katika tabia za binadamu tuna case by case ambazo tunazishughulikia na hata mambo unayozungumzia hivi sasa mengine yako katika utaratibu wa kushughulikiwa. Kwa hiyo, tuvute subira siyo kila kitu ni kutangaza publically lakini kuna mambo kama Serikali tunayafanyia kazi kwa sababu lengo letu ni utii wa sheria bila shuruti uweze kufanyika lakini kufuata utaratibu, sheria na kanuni kwa viongozi na wananchi wote. Ahsante.

Name

Goodluck Asaph Mlinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ulanga

Primary Question

MHE. JOSEPH R. SELASINI (K.n.y. MHE. JESCA D. KISHOA) aliuliza:- Kwa muda mrefu sasa Mkuu wa Wilaya ya Ikingu amekuwa akijichukulia sheria mkononi na kuwanyanyasa wananchi wa Kata za Ighombwe, Iglansoni na maeneo ya Wilaya ya Ikungi. Je, Serikali inaweza kutoa majibu ni mamlaka yapi aliyonayo Mkuu huyo wa Wilaya ya kuwanyanyasa na kuamrisha mali za wananchi kuchomwa moto au kuporwa na Serikali bila utaratibu wowote wa kisheria kwa kisingizio kuwa wanaishi maeneo yasiyoidhinishwa kwa makazi?

Supplementary Question 2

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ukiacha Wakuu wa Wilaya ambao wanafanya vibaya wako Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa wanaofanya vizuri. Kwa mfano, kwa Wakuu wa Mikoa yupo Salum Hapi wa Iringa amekuwa mbunifu kupita kiasi, Ndugu Alexander Mnyeti, Ndugu Mrisho Gambo na Ndugu Paul Makonda... (Makofi/Kicheko)

MWENYEKITI: Mheshimiwa, uliza swali Mheshimiwa Mlinga.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Swali langu ni hili, je, Wizara ina mkakati gani wa kuwaandalia motisha ama tuzo kwa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya hawa ambao wanafanya kazi vizuri?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kama nilivyosema hapo awali mwanzo tulikuwa na matatizo mengi sana, sasa hivi matatizo haya kwa kweli kwa kiwango kikubwa yamepungua sana. Ni kweli nikiri wazi kwamba kuna Wakuu wa Mikoa hivi sasa wanafanya kazi nzuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano, tulianzisha programu ya ujenzi wa viwanda, katika kila mkoa viwanda 100, matarajio yetu ni kupata viwanda 2,600 lakini tumepata viwanda 4,877 ni outstanding performance, lakini kazi hii imesimamiwa na Wakuu wa Mikoa.

Kwa hiyo, agenda ya kuwapa appreciation baadhi ya Wakuu wa Mikoa tumeshaanza kuifanya katika vikao vyetu na juzi-juzi baadhi ya Wakuu wa Mikoa tumeshawakabidhi vyeti vyao kwa jinsi walivyoshiriki katika kuhakikish mambo ya Serikali yanaenda vizuri. Kwa hiyo, hilo tutaendelea kulifanyia kazi, ahsante.

Name

Devotha Methew Minja

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPH R. SELASINI (K.n.y. MHE. JESCA D. KISHOA) aliuliza:- Kwa muda mrefu sasa Mkuu wa Wilaya ya Ikingu amekuwa akijichukulia sheria mkononi na kuwanyanyasa wananchi wa Kata za Ighombwe, Iglansoni na maeneo ya Wilaya ya Ikungi. Je, Serikali inaweza kutoa majibu ni mamlaka yapi aliyonayo Mkuu huyo wa Wilaya ya kuwanyanyasa na kuamrisha mali za wananchi kuchomwa moto au kuporwa na Serikali bila utaratibu wowote wa kisheria kwa kisingizio kuwa wanaishi maeneo yasiyoidhinishwa kwa makazi?

Supplementary Question 3

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kuniona. Si Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya tu ambao hawafanyi vizuri, wapo pia ma-RPC ambao hawafanyi vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, RPC anapotangaza kwamba wananchi wakiandamana atawapiga hadi wachakazwe, hivi kazi ya msingi ya Jeshi la Polisi kwa wananchi wanaolipa kodi ili walipwe mishahara, ni kuchakaza wananchi?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nishukuru sana swali la dada yangu Mheshimiwa Devotha Minja. Nadhani kitu kikubwa kama Taifa, jambo la kwanza tuweke ushirikiano katika kila eneo. Nadhani vyombo vingine vinaongozwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni hasa katika suala zima la mambo ya ndani na sitaki kuviingilia. Kwa hiyo, imani yangu ni kwamba wananchi wote tutafuata utaratibu wa utii wa sheria bila shuruti kwa ajili ya kuepuka migongano mingine ambayo inawezekana siyo ya lazima kwa afya ya Taifa letu.