Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Jerome Dismas Bwanausi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lulindi
Primary Question
MHE. JEROME D. BWANAUSI (K.n.y. MHE. ENG. RAMO M. MAKANI) aliuliza:- (a) Je, nini mpango wa Serikali kukamilisha mradi wa maji safi unaoendelea katika Mji wa Tunduru ili kuwaondolea wananchi hao adha kubwa wanayoipata ya uhaba wa huduma hiyo? (b) Jimbo la Tunduru Kaskazini lina vijiji 92 ambapo taarifa za Serikali na takwimu zinaonesha kiwango cha upatikanaji wa maji kuwa chini sana:- Je, ni lini mpango wa Serikali wa kuongeza kiwango hicho cha upatikanaji wa maji katika vijiji hivyo kufikia kiwango kilichowekwa kwa mujibu wa mipango ya Serikali na Ilani ya CCM itatekelezwa?
Supplementary Question 1
MHE. JEROME D. BWANAUSI: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Swali la kwanza; kwa kuwa asilimia ya upatikanaji wa maji katika Mji wa Tunduru pamoja na vijiji vyake 92 ni wa chini sana; na kwa kuwa Serikali imekuwa ikitoa fedha kidogo kidogo katika mradi mkubwa wa Tunduru:-
Je, Serikali haioni sababu sasa ya kutafuta fedha za kutosha ili mradi huu ukamilike kwa haraka na wananchi waweze kupata maji kwa urahisi?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, vijiji vya Lakalola, Nakachindu, Namwanga, Nangwale, Tupendane, vimekuwa vikikabiliwa na tatizo kubwa sana la maji katika Jimbo la Lulindi pamoja na kule Rivangu na Wakandarasi wako site; kuna OBD and Company na Sing Lyimo Enterprises, lakini tangu wapeleke certificate mwezi Novemba, 2018 hadi sasa Wakandarasi hao hawajapata fedha zao ili kuendelea na kazi:-
Je, nini kauli ya Serikali?
Name
Jumaa Hamidu Aweso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Pangani
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote nimpongeze Mheshimiwa Mbunge. Niwe mkweli, tuna changamoto kubwa sana Tunduru na hata Mkoa wa Ruvuma, tulifanya ziara tukaona changamoto hiyo. Kubwa tunaloliona, tuna ubabaishaji mkubwa sana wa Mhandisi wetu wa Maji wa Mkoa. Sisi kama Wizara tumeshamwondoa na tutaendelea kuwaondoa Wahandisi wote wababaishaji katika Wizara yetu ya Maji.
Mheshimiwa Naibu Spika, kikubwa tunatambua kabisa utekelezaji wa miradi ya maji inategemeana na fedha. Tulikuwa tuna madai zaidi ya shilingi bilioni 88 ya Wakandarasi. Tunashukuru sana Wizara ya Fedha imetupa shlingi bilioni 44, tumeshaanza kuwalipa Wakandarasi na mwezi huu wa Nne mwishoni watatupa shilingi bilioni 44 nyingine katika kuhakikisha tunawakamilishia Wakandarasi madai wanayotudai. Nataka niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge, sisi kama Wizara ya Maji hatutakuwa kikwazo katika kuhakikisha miradi ya maji inakuwa endelevu na kuweza kuwahudumia wananchi. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved