Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Naghenjwa Livingstone Kaboyoka
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. MARY M. NAGU aliuliza:- Maeneo mengi katika Wilaya ya Hanang’ yana matatizo ya maji ingawa Kata za Dirma, Lalaji, Wandela, Gawidu, Bassodesh na Mwanga zina visima vilivyochimbwa licha ya maji kutopatikana:- Je, Serikali ina mikakati gani ya kutatua matatizo ya maji katika wilaya hiyo?
Supplementary Question 1
MHE. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kujibu swali vizuri na naishukuru Serikali kwa jitihada zake zinazoelekezwa Hangang’ hasa ziwe Bassotu.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba niulize maswali mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza, ni kweli visima vimechimbwa, lakini nafikiri ni Wilaya ya peke yake ambayo zimewekwa solar ambazo hazina betri na ni Wilaya ambayo temperature yake iko chini kwa hiyo maji hayapatikani kila wakati. Sasa nataka kujua wakati kwingine kunawekwa solar za betri kwa nini Wilaya ya Hanang’ katika visima mbalimbali vilivyochimbwa kama alivyoeleza Mheshimiwa Naibu Waziri hawakuweka betri hizo na hasa Masakta ambapo ilipangiwa shilingi bilioni 1.2 mpaka leo tatizo liko palepale?
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, Wilaya ya Hanang’ iko kwenye bonde la ufa na kwa hivyo kuna joto chini, kwa hiyo kupata maji kwenye visima ni ngumu sana. Sasa nataka Mheshimiwa Naibu Waziri anieleze kama bwawa linalotakiwa Dirma linachimbwa na bwawa la Gehandu na Gidahababieg linachimbwa kusudi tatizo hilo la ujumla la Hanang’ liweze kukabiliwa?
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali.
Name
Jumaa Hamidu Aweso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Pangani
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze sana mama yangu Mheshimiwa Dkt. Mary Nagu kwa kazi kubwa anayofanya. Ni miongoni mwa wamama ambao wamejitoa kupigania suala zima la maji katika jimbo lake la Hanang.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini swali la kwanza la changamoto ya betri, nimuagize Mhandisi wa Maji wa Mkoa wa Manyara afuatilie kwa haraka ili changamoto hizi tuweze kuzitatua kwa haraka ili wananchi wake waendelee kupata huduma ya maji.
Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo yenye ukame au yaliyopitiwa na bonde la ufa, uchimbaji wa visima imekuwa ni changamoto kubwa sana, mfano Dilma. Sisi kama Wizara ya Maji tumeona haja sasa ya kuchimba mabwawa. Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, sisi kama Wizara ya Maji hatutakuwa kikwazo katika uchimbaji wa mabwawa ili wananchi wake waweze kupata huduma hii muhimu na kuweza kumtua mwanamama ndoo kichwani. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved