Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Jaku Hashim Ayoub
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
House of Representatives
Primary Question
MHE. JAKU HASHIM AYOUB aliuliza:- Kumekuwa na kilio cha uchakavu wa vituo vya polisi kwa upande wa Unguja na Pemba:- (a) Je, ni vituo vingapi vipya vya polisi vilivyojengwa kwa upande wa Unguja na Pemba? (b) Je, vituo hivyo vimejengwa na kampuni gani na ni vigezo gani vilivyoangaliwa katika ujenzi wa vituo hivyo? (c) Je, ni lini Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara watafuatana nami kwenda kuviona vituo hivyo vilivyochakaa?
Supplementary Question 1
MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza nimpe pole sana Mheshimiwa Waziri kwa kuvamiwa Kituo chake cha Polisi cha Madema…
MWENYEKITI: Waheshimiwa, muda wetu umekwisha. Mheshimiwa Jaku.
MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Tarehe 25 Julai, 2017, naomba kunukuu Hansard, “taratibu hizo zilishafanyika kama nilivyokwambia sasa. Tarehe 9 Novemba, “Serikali inatambua deni hilo.” Tarehe 8 Novemba, 2017 mwaka wa Fedha 2017, “Jeshi la Polisi limetenga jumla ya shilingi bilioni 2.2 kwa ajili ya kupunguza madeni ikiwemo mkandarasi.”
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naona ni aibu kwa Serikali yangu kupata aibu na hili deni ni la muda mrefu. Je, Mheshimiwa Waziri, hesabu hata ulipochaguliwa wewe Jimboni kwako ulianzia kwa kura moja ukafika hapa. Kama mimi, Serikali yangu kupata aibu nami ninaipenda niko tayari…
MWENYEKITI: Mheshimiwa, uliza swali.
MHE. JAKU HASHIM AYOUB: …niko tayari kuanza kuchangia shilingi milioni moja kwa ajili ya kituo. Je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kuchukua shilingi milioni moja, kupokea mchango huu ili tufuatane kupeleka deni hilo na hizi hapa? Maana yake deni limeshakuwa la muda mrefu. Yuko tayari kupokea shilingi milioni moja kufuatana nami kupeleka hizi fedha za deni?
Name
Kangi Alphaxard Lugola
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwibara
Answer
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Ilani hii ya CCM ujenzi wa vituo vya Polisi na makazi ya Askari tumeweka utaratibu kwamba tutahusisha wadau. Ninashukuru sana wewe Bungeni kujitokeza kuwa mdau kwa mujibu wa ilani hii. Hivyo naomba mchango wako uuwasilishe kwa Inspekta Jenerali wa Polisi ili tuendelee na ujenzi wa vituo vya Polisi hapa nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ni kweli kabisa kwamba deni la huyu Mkandarasi limekuwa la siku nyingi. Nimhakikishie Mheshimiwa Jaku, ambaye najua akifuatilia jambo lake ni king’ang’anizi, ni moto wa kuotea mbali; na kwa kweli siku siyo nyingi hatutakubali jambo analolisema kwamba Serikali yetu inatiwa aibu. Ndiyo maana Wakandarasi wengi nchini wanapenda kufanya kazi na Serikali na Serikali yetu inalipa madeni yake na deni lake limeshahakikiwa, awe na subira wakati wowote tutaweza kumlipa Mkandarasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Name
Juma Selemani Nkamia
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chemba
Primary Question
MHE. JAKU HASHIM AYOUB aliuliza:- Kumekuwa na kilio cha uchakavu wa vituo vya polisi kwa upande wa Unguja na Pemba:- (a) Je, ni vituo vingapi vipya vya polisi vilivyojengwa kwa upande wa Unguja na Pemba? (b) Je, vituo hivyo vimejengwa na kampuni gani na ni vigezo gani vilivyoangaliwa katika ujenzi wa vituo hivyo? (c) Je, ni lini Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara watafuatana nami kwenda kuviona vituo hivyo vilivyochakaa?
Supplementary Question 2
MHE. JUMA S. NKAMIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Naomba niulize swali moja dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Chemba ni moja kati ya wilaya mpya. Tumeanza kujenga kituo cha Polisi kwa sababu huduma nyingi za Polisi zinapatikana kwenye Wilaya mama ya Kondoa: Je, Serikali ina mchango gani kuhakikisha kwamba tunakamilisha ujenzi wa Kituo cha Polisi pale Chemba ambao tayari tumeuanza?
Name
Kangi Alphaxard Lugola
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwibara
Answer
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Juma Selemani Nkamia, Mshabiki wa Simba namba moja, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jeshi la Polisi katika muundo wake na utoaji wa huduma, tunayo Mikoa 35 ya Kipolisi, tunazo Wilaya 182 za Kipolisi na pia tunazo Tarafa 610 za Kipolisi na tuna Kata na Shehia 4,410. Kwa hiyo, tunao mpango mkakati kuhakikisha kwamba huduma hizi zinakwenda kwenye maeneo yote hayo; na bado tuna mikoa mipya na wilaya mpya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Juma Nkamia kwamba Wilaya ya Chemba ni miongoni mwa wilaya ambazo mikakati yetu ndani ya Jeshi la Polisi tunakwenda kujenga kituo cha Polisi katika Wilaya ya Chemba.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved