Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Amina Saleh Athuman Mollel

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. AMINA S. MOLLEL aliuliza:- Kuna taarifa kwamba nchi ya Kenya inatarajia kutekeleza mpango wa kujenga mabwawa makubwa kwa ajili ya uzalishaji umeme. Kwa kuwa ujenzi huo unatishia ustawi wa uwepo wa Hifadhi ya Taifa Serengeti. Je, Serikali ya Tanzania inachukua hatua gani kuhusu mpango huo?

Supplementary Question 1

MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, namshukuru pia Naibu Waziri kwa majibu mazuri na kwa kuwa Serikali sasa imekiri taarifa hizi, na tunafahamu kwamba siyo kila jambo linalojadiliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki zinakubaliana na tumeshaona kwamba ni tatizo. Je, Serikali inachukua tahadhari gani ili basi jambo hili lisije kutokea kwa sababu litakuwa na madhara makubwa?

Pili, iwapo Serikali ya Kenya itasimama kutekeleza mradi huo; Je, ni madhara gani makubwa ambayo yanatarajiwa hasa kiikolojia na athari zake katika mzunguko wa wanyama, yaani Wild West Movement? Ahsante.

Name

Constantine John Kanyasu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nimpongeze sana kwa swali lake zuri sana, kimsingi uhai wa Mto Mara ndiyo uhai wa Hifadhi ya Serengeti, na ikolojia ya Serengeti inaanzia katika hifadhi zilizoko nchini Kenya. Kwa hiyo, uwepo wa Mto Mara na uhai wa uhifadhi wa Serengeti ni kitu ambacho sisi kama Wizara tunakitilia kipaumbele sana, kwa hiyo, nampongeza sana kwa maswali yake mazuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la kwanza; Je, Serikali inachukua tahadhari gani tumewaelekeza TANAPA kuanza kufuatilia kwa karibu mienendo yoyote ile ambayo inaweza ikapelekea utekelezaji wa mpango huu, na kwa kuwa tunaamini kwamba sisi Serengeti ni Mbuga yetu ambayo tunaitegemea, pia tumewaelekeza kuangalia kama inawezekana kujenga mabwawa ya kuhifadhi maji ili pale utekelezaji wa miradi hii itakapofanyika wanyama wasije wakaathirika kwa ukame.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, ni madhara gani makubwa yanayotegemewa ni kwamba kimsingi wanyama tunaowaona Serengeti wengi katika msimu wao wa mwaka mzima huwa wanatembea katika nchi hizi mbili. Kwa hiyo, Wild West Movement ambayo huwa inatokea Tanzania, huwa inapita mpaka Maasai Mara. Kwa hiyo, iwapo ikolojia hii itaharibiwa, maana yake ni kwamba wanyama hawa wataacha sasa kuwa wana-cross border kuja Tanzania au ku-cross kwenda Kenya na matokeo yake utalii huu ambao ni urithi wa dunia unaweza ukaathirika.