Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Vedastus Mathayo Manyinyi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Musoma Mjini

Primary Question

MHE. VEDASTUS M. MANYINYI aliuliza:- Serikali katika kuhakikisha inapata watumishi bora na wenye sifa iliamua kuwaondoa watumishi wasio na sifa pamoja na wenye vyeti feki, lakini zoezi hilo lilikumbwa na changamoto mbalimbali ambapo Afisa Utumishi aliwaondoa watumishi kwenye payroll bila sababu maalum na walipofuatilia Wizarani walirudishwa kazini:- (a) Je, kwa nini Serikali isiunde timu maalum ili ipite kila Halmashauri kupitia taarifa juu ya zoezi hili ili haki itendeke hasa kwa wale ambao hawana uwezo wa kwenda Wizarani? (b) Wapo watumishi ambao baada ya kuajiriwa kwa kutumia vyeti feki walijiendeleza kielimu zaidi ya Darasa la Saba na wameondolewa kwa kosa la udanganyifu wa vyeti: Je, Serikali haioni kuwa hao ni bora kuliko wale ambao hawakujiendeleza?

Supplementary Question 1

MHE. VEDASTUS M. MANYINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kupata nafasi ili niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri, mkwe wangu, kwa majibu mazuri aliyoweza kunipatia, lakini (a) kwa kuwa Serikali imekiri kwamba kati ya watumishi 15,000 walioondolewa waligundua kwamba watumishi 4,160 waliondolewa kimakosa. Hawa ni wale waliopata nafasi ya kuja Dodoma, Utumishi na kwenda Dar es Salaam kwenye Tume. Wale ambao hawakuwa na uwezo, tafsiri yake ni kwamba wamebaki huko.

Sasa swali; ni lini sasa Serikali itaunda tume ambayo angalau itakwenda kila Halmashauri au Mkoani pale iwaite wale wote waliokumbwa na mkasa huu wa kupoteza ajira waje ili vyeti vyao viweze kuhakikiwa ili wale ambao hawakupata nafasi ya kuja waweze kurudi kazini?

Swali la pili; tunatambua kwamba wako watumishi ambao wamekaa au wametumikia nchi hii katika kipindi kirefu na wengine walibakiza tu mwaka mmoja wastaafu na kwa bahati mbaya wamekumbwa na huo mkasa; Serikali ina mpango gani angalau hata kuwapa kifuta machozi ili waende wakaanze maisha yao huko waliko kuliko kuwaacha kama ilivyowaacha?

Name

Dr. Mary Machuche Mwanjelwa

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mbeya Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia sana suala la watumishi wa Umma, hususan wale ambao walikuwa wameandika taarifa zisizokuwa na ukweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza kujibu swali lake la kwanza; kwanza kabisa naomba nimwambie Mheshimiwa Mbunge na kwa faida ya Watanzania wengine na Watumishi wa Umma wote kwamba Serikali ilishafanya zoezi la ufuatiliaji kwa zaidi ya asilimia 95 na hilo zoezi limeshakamilika. Wale watumishi wote ambao waliandika taarifa zao siyo sahihi katika personal records au kwenye OPRAS, naomba niliambie Bunge lako Tukufu kwamba kama walidanganya watakosa stahiki zao zote kwa sababu Kanuni ya Utumishi wa Umma, kile kifungu D.12 kinasema mtumishi yeyote ambaye anaandika taarifa za uongo hataruhusiwa kuwa Mtumishi wa Umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Serikali pia ilitoa msamaha hadi tarehe 31 Desemba, 2017, kwamba wale wote ambao walikuwa wamejiendeleza, basi walete taaifa zao kwenye Ofisi yetu ya Utumishi maana ilishatoa msamaha ili taarifa zao ziweze kuingia na waweze kurudi kazini. Kwa hiyo, zaidi ya watumishi 500 wamesharejeshwa na wale ambao walijiendeleza baada ya muda huo basi waweze kutuletea vyetu vyao tuweze kuhakiki na waweze kurudi kazini. Ahsante.

Name

Dr. Stephen Lemomo Kiruswa Mamasita

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Longido

Primary Question

MHE. VEDASTUS M. MANYINYI aliuliza:- Serikali katika kuhakikisha inapata watumishi bora na wenye sifa iliamua kuwaondoa watumishi wasio na sifa pamoja na wenye vyeti feki, lakini zoezi hilo lilikumbwa na changamoto mbalimbali ambapo Afisa Utumishi aliwaondoa watumishi kwenye payroll bila sababu maalum na walipofuatilia Wizarani walirudishwa kazini:- (a) Je, kwa nini Serikali isiunde timu maalum ili ipite kila Halmashauri kupitia taarifa juu ya zoezi hili ili haki itendeke hasa kwa wale ambao hawana uwezo wa kwenda Wizarani? (b) Wapo watumishi ambao baada ya kuajiriwa kwa kutumia vyeti feki walijiendeleza kielimu zaidi ya Darasa la Saba na wameondolewa kwa kosa la udanganyifu wa vyeti: Je, Serikali haioni kuwa hao ni bora kuliko wale ambao hawakujiendeleza?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. STEVEN L. KIRUSWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kuniona. Naomba kuuliza kuhusu watumishi waliochishwa kazi kwenye hili zoezi wenye vyeti vya Darasa la Saba wakaenda chuo; kwa mfano kuna waliokwenda Chuo cha Simanjiro cha Mifugo wakapata vyeti, waka- perform vizuri wakaenda kusoma Diploma ya Udaktari wa Mifugo katika chuo cha Serikali kule Tengeru, lakini baada ya zoezi kupita walipogundulika tu kwamba hawana cheti cha form four – lakini hawajadanganya – wakaachishwa kazi.

Je, Serikali inaweza kutoa tamko gani kuhusu hawa ambao wanaona kwamba wameonewa?

Name

Dr. Mary Machuche Mwanjelwa

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mbeya Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza lazima tukumbuke kwamba tarehe 20 Mei, 2004, baada ya hapo wale wote ambao walikuwa wametoa taarifa zisizo sahihi tulitoa msamaha hadi tarehe 31 Desemba, 2017 kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi na wale wote waliojiendeleza, kwa mfano katika masuala ya recategorization.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme, Serikali tunasisitiza, tunathamini, tunaheshimu recategorization kwa wale wote wanaojiendeleza kimasomo. Nimesema kwamba hadi hiyo tarehe 31 Desemba, 2017 kama walijiendeleza na vyeti vyao viko sahihi, watuletee Utumishi tutahakiki watarejeshwa kazini. Ahsante.

Name

Conchesta Leonce Rwamlaza

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. VEDASTUS M. MANYINYI aliuliza:- Serikali katika kuhakikisha inapata watumishi bora na wenye sifa iliamua kuwaondoa watumishi wasio na sifa pamoja na wenye vyeti feki, lakini zoezi hilo lilikumbwa na changamoto mbalimbali ambapo Afisa Utumishi aliwaondoa watumishi kwenye payroll bila sababu maalum na walipofuatilia Wizarani walirudishwa kazini:- (a) Je, kwa nini Serikali isiunde timu maalum ili ipite kila Halmashauri kupitia taarifa juu ya zoezi hili ili haki itendeke hasa kwa wale ambao hawana uwezo wa kwenda Wizarani? (b) Wapo watumishi ambao baada ya kuajiriwa kwa kutumia vyeti feki walijiendeleza kielimu zaidi ya Darasa la Saba na wameondolewa kwa kosa la udanganyifu wa vyeti: Je, Serikali haioni kuwa hao ni bora kuliko wale ambao hawakujiendeleza?

Supplementary Question 3

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali moja tu la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wako maredeva ambao waliondolewa katika mfumo wa Serikali kwamba wamemaliza Darasa la Saba, kwa hiyo hawastahili kuwa madereva. Naomba kuiuliza Serikali, ni kigezo kipi ambacho kilitumika kuona kwamba dereva wa Darasa la Saba anaweza kuendesha gari vibaya kuliko yule wa Darasa la 12?

Name

Dr. Mary Machuche Mwanjelwa

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mbeya Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba niliambie Bunge lako Tukufu kwamba Serikali pia inawajali hata hao madereva wa Darasa la Saba. Naomba niliambie Bunge lako Tukufu kwamba madereva wote wale wa Darasa la Saba ambao walikuwa wamebainika kwamba vyeti vyao viko safi na taarifa zao ziko safi na waliandika ukweli, wapo kazini na wanaendelea na kazi kama kawaida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.