Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Deogratias Francis Ngalawa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ludewa
Primary Question
MHE. EDWIN M. SANNDA (K.n.y. MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA) aliuliza:- Serikali iliahidi kulipa fidia wananchi walioachia maeneo yao kupisha miradi ya makaa ya mawe, Mchuchuma na Liganga lakini mpaka sasa hawajalipwa:- (a) Je, ni lini Serikali italipa fidia hizo ili wananchi husika waendelee na shughuli nyingine za kiuchumi? (b) Je, kwa nini Serikali haitoi mrejesho pindi panapotokea mkwamo? (c) Je, Serikali inaweza kuthibitisha kuwa miradi hiyo itaanza kutekelezwa kama ilivyoahidi Bungeni?
Supplementary Question 1
MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, Mradi wa Mchuchuma na Linganga umekuwa ukizungumzwa kwa muda mrefu sana kipindi ambacho sasa mpaka wananchi na Watanzania kwa ujumla wanakata tamaa. Sasa je, Serikali haioni kwamba sasa hivi hii hela ya fidia ingeichukua yenyewe badala ya kumwachia mwekezaji na watu wetu wakapata fidia hiyo mapema.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili tumeona jitihada za Serikali kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa barabara ya kutoka Mkiu - Liganga mpaka Madaba na ya kutoka Mchuchuma mpaka Liganga kilometa 70. Je, ujenzi hasa wa lami na kuhakikisha kwamba maeneo hayo yanaweza kupitika yataanza lini?
Name
Eng. Stella Martin Manyanya
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nyasa
Answer
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kabla sijaendelea na maswali ya nyongeza kwa umuhimu wake kwa niaba ya wanaviwanda pamoja na Wizara yetu ya Viwanda kwa ujumla napenda kutoa pole kwa msiba mkubwa uliotupata kupitia kifo cha mwanakiwanda au mfanyabiashara wetu Mkuu ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation, Dkt. Reginald Mengi. Mwenyezi Mungu amrehemu na roho yake aiweke mahali pema peponi. Amina.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianzia swali la kwanza kuhusu Serikali uwezekano wa kulipa fidia, tunapotathmini mradi huu kuna njia mbili; ya kwanza ni kwa kumtumia mwekezaji aweze kulipa fidia, lakini Serikali inapokuwa na uwezo inaweza ikalipa yenyewe. Kwa hiyo, katika kuangalia mradi huu ambao una umuhimu sana kwa Taifa letu kutokana na rasilimali zilizoko pale, Serikali inaangalia uwezekano pia wa yenyewe kuweza kulipa fidia endapo itawezekana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, kuhusiana na barabara kujengwa kwa kiwango cha lami, hayo yote yapo katika mchakato huo wa Serikali kujipanga ili kuwezesha mradi huu ufanyike kwa tija na kwa manufaa mapana ya Taifa.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, napenda tu niongezee kwamba Serikali inayo mpango wa kujenga kiwango cha lami kuzingatia kama Mheshimiwa Mbunge anavyozungumza katika maeneo ambayo tumeya-alert kwa ajili ya uchimbaji wa makaa ya mawe na chuma. Tumemaliza usanifu wa barabara kutoka Madaba kwenda Mkiu kilomita mia moja kumi na mbili, lakini pia eneo la barabara ya kutoka Mchuchuma kwenda Liganga, ziko kilometa 72 tumesanifu, Serikali ikipata fedha maeneo hayo muhimu tutajenga kwa kiwango cha lami.
Name
Sophia Hebron Mwakagenda
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. EDWIN M. SANNDA (K.n.y. MHE. DEOGRATIAS F. NGALAWA) aliuliza:- Serikali iliahidi kulipa fidia wananchi walioachia maeneo yao kupisha miradi ya makaa ya mawe, Mchuchuma na Liganga lakini mpaka sasa hawajalipwa:- (a) Je, ni lini Serikali italipa fidia hizo ili wananchi husika waendelee na shughuli nyingine za kiuchumi? (b) Je, kwa nini Serikali haitoi mrejesho pindi panapotokea mkwamo? (c) Je, Serikali inaweza kuthibitisha kuwa miradi hiyo itaanza kutekelezwa kama ilivyoahidi Bungeni?
Supplementary Question 2
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kama ilivyo kwa wananchi wa Ludewa ni lini Serikali itaweka na kuharakisha utekelezaji wa kuwalipa fidia wale wananchi wa Wilaya ya Kyela waliopisha mradi wa Boarder Post? Ahsante.
Name
Elias John Kwandikwa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ushetu
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Mwenyekiti napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mwakagenda kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. Magufuli alipokuwa ziara Kyela ametoa maelekezo ili tuweze kuwalipa mara moja wananchi katika eneo hili, nimwarifu tu Mheshimiwa Mbunge, nami nimeongea na wananchi hawa baada ya maelekezo ya Mheshimiwa Rais na tunalifanyia kazi suala hili ili tuweze kuwalipa wananchi hawa. Kwa hiyo Mheshimiwa Mwakagenda avute subira, sisi tumejipanga kama Serikali na kwa sababu Mheshimiwa Rais pia amekuwa na concern hiyo, wananchi watapata haki zao mara moja.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved