Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Shabani Omari Shekilindi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lushoto
Primary Question
MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI aliuliza:- Hospitali ya Wilaya ya Lushoto ni ya muda mrefu na hata ujenzi wa majengo yake ni wa kizamani ambao hauendani na utoaji huduma na Serikali ina utaratibu wa kukarabati na kuongeza majengo katika Hospitali za Wilaya:- Je, ni lini Hospitali ya Wilaya ya Lushoto itakarabatiwa?
Supplementary Question 1
MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Waziri yenye kutia moyo lakini nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwa Serikali ina mpango wa kukarabati Vituo vya Afya na Hospitali za Wilaya na kutoa vifaatiba. Je, ni lini sasa itatoa X-ray mashine katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto ili kupunguza msongamano au usumbufu wa wananchi wangu kutoka Lushoto kwenda mpaka Tanga hadi Muhimbili?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Jimbo la Lushoto lina Kata 15 na Kituo cha Afya kimoja tu. Wananchi wa Kata za Gare na Ngwelo kwa nguvu zao wenyewe wameanza kujenga maboma hayo ya Vituo vya Afya. Je Serikali ina mpango gani wa kuongeza fedha au wa kuwapatia fedha zile ambazo zinatolewa shilingi milioni 400 kwa ajili ya kujenga vituo hivyo? Nia na madhumuni ni kupunguza msongamano mkubwa uliopo katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto.
Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Shekilindi, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la kwanza juu ya uwepo wa X-ray, naomba nimtoa wasiwasi Mheshimiwa Mbunge pamoja na wananchi wa Lushoto kwamba mchakato uko kwenye hatua za mwisho kupitia MSD. Muda si mrefu X-ray ile itapatikana ili wananchi wa Lushoto na maeneo ya jirani waweze kupata huduma ya vipimo hivyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini katika swali lake la pili, naomba nimpongeze yeye mwenyewe na Mheshimiwa Shangazi wamekuwa wakifuatilia sana kuhusiana na Hospitali ya Lushoto. Naomba pia niwapongeze wananchi ambao wameanza ujenzi wa Kituo cha Afya. Hakika pale ambapo wananchi wanaanza Serikali inawaunga mkono mara moja. Naomba nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwa kadri bajeti itakavyoruhusu na fedha ikipatikana tunahakikisha tunapeleka maeneo ambayo tayari nguvu ya wananchi ilishakuwepo. Mchakato utakavyokamilika hakika hatutawasahau wananchi wa eneo alilolitaja.
Name
Mary Pius Chatanda
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Korogwe Mjini
Primary Question
MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI aliuliza:- Hospitali ya Wilaya ya Lushoto ni ya muda mrefu na hata ujenzi wa majengo yake ni wa kizamani ambao hauendani na utoaji huduma na Serikali ina utaratibu wa kukarabati na kuongeza majengo katika Hospitali za Wilaya:- Je, ni lini Hospitali ya Wilaya ya Lushoto itakarabatiwa?
Supplementary Question 2
MHE. MARY P. CHATANDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Korogwe Mji tumekabidhiwa Hospitali ya Wilaya Magunga kutoka Korogwe Vijijini. Kwa bahati mbaya sana ina wodi moja tu ambayo wanalala wajawazito pamoja na wale waliojifungua. Je, Serikali itakuwa tayari kusaidia tupate fedha angalau tuweze kujenga wodi ya wajawazito na watoto?
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nimpongeze Naibu Waziri kwa majibu mazuri sana ya ndugu yangu Mheshimiwa Shekilindi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiri wazi kwamba tumefika katika Hospitali ile anayoizungumzia Mheshimiwa Mama Chatanda mara kadhaa licha ya upungufu wa wodi lakini hospitali ile imekuwa ya wahenga sana, imekuwa kongwe. Kwa hiyo, ni mpango wetu kuhakikisha tunafanya maboresho ya hospitali za zamani. Nimhakikishie Mheshimiwa Chatanda kwamba licha ya wodi hizo lakini tutaangalia kwa jicho lingine jinsi gani tufanye hospitali ile ifafanane sasa na Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
Name
Esther Nicholus Matiko
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI aliuliza:- Hospitali ya Wilaya ya Lushoto ni ya muda mrefu na hata ujenzi wa majengo yake ni wa kizamani ambao hauendani na utoaji huduma na Serikali ina utaratibu wa kukarabati na kuongeza majengo katika Hospitali za Wilaya:- Je, ni lini Hospitali ya Wilaya ya Lushoto itakarabatiwa?
Supplementary Question 3
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Hospitali ya Wilaya ya Mji wa Tarime ambayo kiukweli inatoa huduma kama Hospitali ya Wilaya au ya Mkoa naweza nikasema na Kanda Maalum Tarime Rorya, Mheshimiwa Naibu Waziri alitembelea na akaona ni jinsi gani inaelemewa kwa utoaji wa huduma. Hivi ninavyoongea chumba cha kuhifadhia maiti kwa maana ya mortuary kwanza ni kifinyu lakini pia mashine yake kwa maana ya compressor haifanyi kazi na wale ndugu zetu ambao tunawahifadhi pale wakikaa muda mdogo wanaharibika. Nataka kujua commitment ya Serikali ya kuhakikisha kwamba inasaidia ukarabati au upanuzi wa mortuary ikiwemo kusaidia hiyo mashine ya compressor kwa sababu Halmashauri ya Mji wa Tarime haina kipato cha kutosha. Ahsante.
Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la Mheshimiwa Esther Matiko, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ukweli usiopingika kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge nilipata fursa ya kutembelea hospitali ile ambayo ina congestion kubwa na bahati nzuri nilipata fursa nikiambata na Mheshimiwa Waziri Mkuu. Maelekezo ambayo yalikuwa yametolewa, kwanza ni kuhakikisha kwamba dawa za kutosha zinatolewa ili kukidhi haja kwa sababu wananchi ni wengi wanaopata huduma pale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hili ambalo amelisema kuhusiana na chumba hicho cha kuhifadhia maiti ambacho mashine imeharibika kiasi kwamba sasa mwili unaharibika ndani ya muda mfupi, naomba seriously tukitoka hapa tuwasiliane na Mheshimiwa Mbunge ili tuone hatua za haraka za kuchukua kuhakikisha kwamba mochwari ile inafanya kazi.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved