Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mashimba Mashauri Ndaki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Magharibi

Primary Question

MHE. MASHIMBA M. NDAKI aliuliza:- Usanifu wa Mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Miji ya Bisega, Bariadi, Itilima, Meatu na Maswa umekamilika kwa kiasi kikubwa lakini utanufaisha watu wa Maswa Mjini na baadhi ya vijiji katika Jimbo la Maswa Mashariki na kuliacha Jimbo la Maswa Magharibi bila ya maji ya uhakika:- Je, kwa nini Serikali isichukue maji kutoka mji wa Algudu ambako tayari maji yameshafika na umbali ni mfupi ili Wananchi wa Kata za Malampaka, Mataba, Nyabubunza, Badi, Shishiyu, Masela, Sengwa, Jija, Kadoto, Mwanghondoli, Mwabayamla, Isanga, Busagi na Buchambi waweze kunufaika?

Supplementary Question 1

MHE. MASHIMBA M. NDAKI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa muda niulize maswali mawili ya nyongeza. Nishukuru pia kwa majibu ya Mhshimiwa Waziri lakini nilikuwa na ushauri mmoja na swali moja. Ushauri kwa kuwa Serikali imeamua kutoa maji kutoka kwenye maziwa makuu kama Ziwa Victoria na maziwa mengine ili kuwapa wananchi wake maji ya kutosheleza ingekuwa vizuri sasa inapobuni miradi hii ikafikiria kuwapa maji watu wanaohusika, lakini pia ikafikiria mbele uhitaji wa maji jinsi ulivyo mkubwa kwenye nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano Mradi wa Maji wa Ngudu kama ungebuniwa vizuri ungeweza kabisa kutoa maji kwenye vijiji na kata nilizozitaja. Kwa hivyo inapobuni miradi ifikirie kupeleka mradi kwa watu wengi zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali kwa kuwa pia nilishapeleka andiko kwaajili ya kupata maji ya Ziwa Victoria kutoka Wilaya Kishapu kwenda Kata ya Sengwa yenye vijiji vya Seng’wa, Mwanundi, Mandela, Mwabomba na Seng’wa yenyewe. Ni lini sasa wizara itaweka pesa kwenye mradi huu ili uweze kutekelezwa?

Name

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkoani

Answer

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya ziada ya Mheshimiwa Ndaki kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ni ushauri tumeupokea ambapo na ni mipango ya Serikali kwamba tukianza kutengeneza miradi mikubwa lazima tuangalie maeneo ya mbali ili kuhakikisha wananchi wengi wanapata maji safi na salama na ndio maana sasa hivi miradi yote tunayojenga tunaochukua maji kutoka Ziwa Victoria tunatoa maoteo au tunapeleka maji mpaka kilometa 12 inapopita bomba kuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili ni kweli tumepokea andiko lake na andiko hilo lina gharama takribani shilingi bilioni kwa ajili ya kutoa maji kwenye bomba kuu la Kashuasa na kupeleka maji kwenye vijiji vya Manawa, Sengwa, Mwabomba, Mandale na Mwanundi ambao tunalipitia sasa hivi na mara baada ya kulipitia tutafanya utaratibu wa manunuzi ili tuhakikishe kwamba wananchi wa maeneo hayo wanapata maji safi na salama kutoka Bomba kuu la KASHUASA.