Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Primary Question

MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza:- Kwa muda mrefu sasa Wilaya ya Kilindi haina Hospitali ya Wilaya lakini wanayo Hospitali ya Rufaa inayomilikiwa na Kanisa la KKKT, lakini watumishi wote na huduma zote za Hospitali hiyo zinagharamiwa na Halmashauri ya Wilaya (DED) na wao KKKT ni wamiliki wa majengo:- Je, Serikali haioni imefika wakati wa kufanya makubaliano ya kununua Hospitali hiyo ili kupunguza gharama kwa Serikali ya kujenga Hospitali ya Wilaya?

Supplementary Question 1

MHE. OMARI M. KIGUA: Ahsante Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza namshukuru Naibu Waziri kwa majibu mazuri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli kabisa nami naungana na Serikali kwamba kuna umuhimu wa Serikali kushirikiana na sekta binafsi katika kuwaletea Watanzania huduma. Pamoja na hali hiyo, zimejitokeza changamoto nyingi sana sana katika Hospitali hii ya KKKT mojawapo ni suala la utawala.

Swali: Je, Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari sasa kuangalia utaratibu ulio mzuri ili dhana hasa ya ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi iweze kufikiwa?

Swali la pili, kwa kuwa Kilindi haina Hospitali ya Wilaya: Je, Serikali iko tayari sasa kuitengea fedha Wilaya ya Kilindi ili iweze kupata Hospitali ya Wilaya? Ahsante.

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni azma na lengo la Serikali kuhakikisha kwamba zile hospitali ambazo tunashirikiana katika kutoa huduma kwa maana ya DDH, suala la utawala bora inakuwa ni kipaumbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawe ni shuhuda kwamba katika swali lake amesema kuna tatizo la utawala. Sasa ni vizuri Mheshimiwa Kigua tukitoka hapa tuelekezane hasa tatizo ni nini ili tuweze kutoa ufumbuzi ili wafanyakazi nao waweze kuona ni sawa na ambavyo wanafanya katika hospitali zetu za Wilaya. Kwa sababu suala la kuwa na utawala bora ni jambo la msingi kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Kigua atakubaliana na Serikali kwamba azma ya kuhakikisha kwamba hospitali zinajengwa katika maeneo yote ambayo Halmashauri hazina Hospitali za Wilaya inafikiwa. Kwa kuanzia, yeye mwenyewe ni shuhuda, katika bajeti ambayo Bunge lako Tukufu limetupitishia, tumeweza kuwatengea kwa kuanzia shilingi milioni 200 kwa ajili ya kujenga Kituo cha Afya cha Msente. Naamini baada ya kuhakikisha kwamba tunakamilisha ujenzi wa hospitali 67 tulizoanza nazo na 52, hakika naomba nimtoe shaka kwamba na Kilindi tutakwenda.