Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Amina Nassoro Makilagi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. AMINA N. MAKILAGI aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuboresha miundombinu ya Kituo cha Afya cha Kiagata kwani Wananchi wote wa Wilaya ya Butiama wanategemea Kituo hicho?
Supplementary Question 1
MHE. AMINA N. MAKILAGI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri, Kaka yangu Kandege, pamoja na kuipongeza Serikali kwa kazi nzuri sana iliyofanya ya kuboresha hiki kituo muhimu cha Kiagata ambacho sasa kinatoa huduma kwa kiwango cha ufanisi, na pia kuishukuru Serikali kwa kazi nzuri sana iliyofanya ya kujenga vituo zaidi ya tisa katika Mkoa wa Mara, nina maswali mawili ya nyongeza kama ifuayavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; kwa kuwa kituo cha Kiagata na hata hospitali ya Wilaya ya Butiama ina upungufu wa wataalam kwa kiwango cha asilimia 70, kwamba pia lipo tatizo kubwa la wataalam wa mionzi lakini vilevile hakuna x-ray kwa Wilaya nzima ya Bitiama ikiwemo hospitali ya Wilaya na hata kituo cha Kiagata.
Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha inapeleka wataalam katika hospitali ya Butiama na Kituo cha Kiagata na hasa kipaumbele kikiwa ni wale watalam wa mionzi kwa ajili ya wakina Mama?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa Wilaya ya Butiama kwa mujibu wa sensa ina watu zaidi ya 200,003 na Butiama ni Wilaya ya kazi, watu wanakula wanashiba, population ya watu inaongezeka.
Vilevile kwa kuwa Wilaya ya Butiama ina kata 18 na ina vitongoji 370 lakini Kituo cha Afya ni kimoja tu cha Kiagata ambacho kinahudumia hata wananchi wote wa Wilaya y Butiama; Tarafa ya Makongoro iko mbali na Kiagata, Wananchi wa Makongoro wanapata shida sana kwenda Kituo cha Afya cha Kiagata;
(i) Ni mkakati gani sasa wa Serikali wa kuboresha Kituo cha Bisumwa ili kiwe sasa kituo cha afya, ili kisaidie Kata saba?
(ii) Serikali ina mkakati gani wa kuboreshga Zahanati ya Kirumi ili sasa isaidie Kata sita?
(iii) Na Serikali ina mkakati gani wa kuboresha Zahanati ya Buhemba ili iweze kusaidia wananchi wa Wilaya ya Butiama?
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu maswali mawili ya Mheshimiwa Amina Makilagi kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba uniruhusu nipokee pongezi ambazo ametoa kwa Serikali ya Awamu ya Tano kwa kazi inayofanya ya kupeleka huduma za afya jirani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la kwanza, anaongelea suala zima la uharaka wa kuhakikisha kwamba wanakuwepo wataalam, na hasa wataalam wa mionzi, ili kazi nzuri iliyofanyika Kituo cha Kiagata iweze kutoa matunda. Naomba nitumie fursa hii kumuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya, miongoni mwa wataalam waliopo ateue angalau mtaalam mmoja akasomee kazi ya mionzi ili huduma ianze kutolewa ili huduma ianze kutolewa wakati Serikali inafikiria kupeleka wengine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ametaja kituo cha afya lakini na zahanati kama tatu, sina uhakika kama ni swali moja lakini naomba itoshe tu nimambie Mheshimiwa Makilagi, kazi kubwa, nzuri ambayo anaipigania kuhakikisha hasa akina mama wanapata huduma ya afya, sisi kama Serikali tuko pamoja na yeye.
Naomba nitoe wito kwa halmashauri kuhakikisha kwamba maombi yote ambayo Mheshimiwa Amina Makilagi ameyatoa hapa yanazingatiwa katika bajeti hii ambayo inaandaliwa na sisi Serikali Kuu hakika hatutamuangusha. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved