Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Daimu Iddi Mpakate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kusini

Primary Question

MHE. DAIMU I. MPAKATE aliuliza:- Jimbo la Tunduru Kusini lina changamoto ya maji kutokana na mabadiliko ya tabianchi:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuchimba visima virefu na vifupi katika kata ya Tuwemacho, Mchuluka, Mchoteka, Mbati, Marumba, Wenje, Nasomba, Namasakata na Lukumbule.

Supplementary Question 1

MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda kumshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri. Na ninamshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kutembelea katika kijiji cha Mbesa aliahidi kisima kirefu amechimba, amekwenda kuangalia na sasa ameahidi kutoa milioni 200 kwa ajili ya kufanya ule mradi kukamilike vizuri. Vilevile tunawashukuru wafadhili wetu waliojenga visima 72 na wengine wamejenga visima 90 katika Jimbo la Tunduru Kusini. Na nina maswali mawili ya nyongeza.

Kwa kuwa mradi wa Mbesa, mradi wa Lukumbuli ambao ulikamika miaka mitatu iliyopita na mradi wa wanalasa ambao ulikamilika zaidi miaka 9 iliyopita haufanyi kazi kutokana na tatizo la kutumia mafuta ya diesel ambayo wananchi wameshindwa kutumia.

Je, Serikali ina mpango gani wa kufunga solar ili wananchi waweze kutumia kwa ukamilivu?

Kwa kuwa katika mradi wa Kijiji cha Mtina uliokamika mwaka moja uliopita umeshindwa kufanya kazi vizuri kutokana na panel solar zilizopo pale kutokutosheleza kusukuma maji kwa ajili ya kupeleka kwa wananchi.

Je, Serikali haioni haja yakuongeza solar panel katika mradi ule ili uweze kuhudumia wananchi wa Mtina ipasavyo?

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kiukweli ni miongoni mwa Wabunge wanafanya kazi kubwa sana, na niseme hili ni baba lao kwa eneo la Tunduru Mungu akubariki sana. Lakini kikubwa ninachotaka kukisema watalamu wetu kwa maana ya WARUSA pamoja na wizara hawana kisingizio tena, utekelezaji wa miradi ya maji inategemeana na fedha, tumepata fedha kwa mikoa 17 zaidi ya bilioni 119. Hata katika Jimbo lako la Tunduru tumeshapeleka bilioni 1.3 hizi fedha ni kwa ajili ya kwenda kutatua changamoto za miradi ya maji. Ni mtake mhandishi wa maji wa Tunduru Kusini katika kuhakikisha anatumia changamoto hizi ili kukarabati na wananchi wako waweze kupata huduma ya maji safi na salama na yenye kutosheleza. Ahsante sana.