Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Juma Selemani Nkamia
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chemba
Primary Question
MHE. JUMA S. NKAMIA ali uliza:- Je, Serikali imekusanya kiasi gani cha kodi kutoka kwa makocha na wachezaji wa kigeni wanaofanya kazi nchini katika mwaka wa fedha 2017/2018?
Supplementary Question 1
MHE. JUMA S. NKAMIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya dada yangu Mheshimiwa Dkt. Ashatu, nina maswali mawili tu madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; malipo ya wachezaji na makocha wengi wa kigeni hapa Tanzania yanafanywa kiholela, hakuna mfumo rasmi:-
(a) Je, Serikali inatambuaje kwamba fulani kalipa na fulani hajalipa?
(b) Nchi zilizoendelea kama Uingereza, kodi ni jambo muhimu sana kwa wachezaji wa mpira wa miguu na hakuna kukwepa. Je, Serikali hapa Tanzania ina mkakati gani wa kuhakikisha kwamba vilabu vya ligi daraja la Premier na ligi daraja la kwanza wanapopata ajira kwenye vilabu hivi wanalipa kodi?
Name
Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Kondoa
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la kwanza kujua nani kalipa na nani hajalipa kama nilivyosema, kulingana na Sheria ya Kodi ya Mapato ya Mwaka 2004, kila mtu anayepata mapato ndani ya Taifa letu anastahili kulipa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni jukumu la mwajiri kwenda kut oa taarifa Mamlaka ya Mapato Tanzania ya waajiriwa wake alionao wanaotakiwa kulipa kodi hiyo. Kwa hiyo, niwatake tu timu zetu zote ambazo zinaajiri makocha na wachezaji kutoka nje ya nchi ; kwenye mikataba yao, maana msingi wa kulipa kodi ya mapato na kodi ya ajira, kwanza kodi ya mapato ni lazima mlipaji yule awe ni mkazi ndani ya Taifa letu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunavyofahamu, pia kwa kodi hii ya mapato, kila mgeni akifikisha zaidi ya miezi sita anahesabika ni local resident na anatakiwa alipe kodi hiyo na mwajiri wake, anatakiwa kutoa taarifa hiyo ili kodi hiyo iweze kulipwa.
Mheshimiwa Mwenyeki ti, kwa hiyo, ni mhaki kishie tu kaka yangu kwamba waajiriwa wote wanatakiwa kulipa kodi hii kulingana na Sheria za Taifa letu zinavyoelekeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuh usu swali lake la pili kwamba wanalipa kiholela n a wengin e yawezekana wan alipwa fedha hizi mkononi ; kama nilivyosema, ni jukumu la mwajiri kutoa taarifa ya nani analipwa nini ndani ya klabu yake ndani ya taasisi yake na ndani ya kampuni yake ili kodi zote zinazostahili kulipwa na hasa kodi ya mapato ambayo ni ngumu kulipika iweze kulipwa kama sheria zetu zinavyotakiwa kutekelezwa kwa vitendo.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved