Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
James Kinyasi Millya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Simanjiro
Primary Question
MHE. JAMES K. MILLYA aliuliza:- Kuna mradi mkubwa wa kutoa maji kutoka Mkoa wa Kilimanjaro kuelekea Arusha Mjini, mradi huu unapitia kwenye mipaka ya Wilaya ya Simanjiro Kata za Naisinyai na Mererani. (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha Wananchi wa Kata hizo wanapatiwa huduma hiyo inayopita kwenye maeneo yao; (b) Mheshimiwa Rais alipokuwa akizindua ujenzi wa barabara ya kilometa 14 toka KIA hadi Mererani aliwaahidi Wananchi wa Mererani na Naisinyai kwamba atawakumbuka kwenye kuondoa adha ya maji; Je, Serikali imejipangaje kutimiza ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais?
Supplementary Question 1
MHE. JAMES K. MILLYA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali. Maeneo niliyosema ya Naisinyai na Mererani ni maeneo ambayo tunapata madini ya tanzanite, ni aibu sana kama pamoja na rasilimali hiyo kubwa maeneo yale hayana maji. Sasa Mheshimiwa Naibu Waziri anihakikishie kwamba bomba lile litakapopita Vijiji vya Lengasti, Mihiye, Oloshonyoke kama ambayo umesema yatapata maji.
Mheshimiwa Spika, nimuombe Mheshimiwa Naibu Waziri, kuna bomba la maji kutoka Ruvu kwenda Olekosmet la takribani bilioni 41, niishukuru Serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuleta mradi huu. Je, yupo tayari kuongozana na mimi kukagua mradi huu ili ifikapo Mei mwakani kama ambavyo Serikali imeahidi mara zote mradi huu uweze kukamilika na wananchi wapate maji safi na salama kwa ajili ya mifugo na watu wa Simanjiro?. (Makofi)
Name
Jumaa Hamidu Aweso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Pangani
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kazi kubwa anayoifanya, kiukweli ni miongoni mwa Wabunge ambao wanafanya kazi kubwa sana na nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge anatosha mpaka chenji inabaki.
Mheshimiwa Spika, kikubwa ambacho ninataka kukisema, tunatambua maji ni uhai na sisi kama Wizara ya Maji eneo lile la Mererani tulishachimba kisima kikubwa lakini changamoto ambayo tuliiona ni kuwepo kwa fluoride kwa kiwango kikubwa sana. Sasa tunatekeleza mradi zaidi ya bilioni 520 katika Jiji la Arusha na baadhi ya vyanzo hivi vya maji vipo katika Jimbo lake. Ninachotaka kumhakikishia bomba kuu lile litakapopita katika maeneo yale ya Mererani na Naisanyi yote yatapatiwa huduma hii ya maji.
Mheshimiwa Spika, kuhusu kwenda katika Jimbo lake la Simanjiro katika ule mradi wa Olekosmet, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba baada ya Bunge nipo tayari kuongozana nae katika kuhakikisha tunafika katika mradi ule. (Makofi)
Name
Flatei Gregory Massay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Vijijini
Primary Question
MHE. JAMES K. MILLYA aliuliza:- Kuna mradi mkubwa wa kutoa maji kutoka Mkoa wa Kilimanjaro kuelekea Arusha Mjini, mradi huu unapitia kwenye mipaka ya Wilaya ya Simanjiro Kata za Naisinyai na Mererani. (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha Wananchi wa Kata hizo wanapatiwa huduma hiyo inayopita kwenye maeneo yao; (b) Mheshimiwa Rais alipokuwa akizindua ujenzi wa barabara ya kilometa 14 toka KIA hadi Mererani aliwaahidi Wananchi wa Mererani na Naisinyai kwamba atawakumbuka kwenye kuondoa adha ya maji; Je, Serikali imejipangaje kutimiza ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais?
Supplementary Question 2
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Hali ya ukosefu wa maji iliyopo Simanjiro inafanana kabisa na Mbulu Vijijini, Mheshimiwa Naibu Waziri umefika Mbulu Vijijini. Je, miradi hii ya maji na kisima cha Hyadom ulichotoa ahadi nini unatimiza, ahsante. (Makofi)
Name
Jumaa Hamidu Aweso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Pangani
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninachotaka kumhakikishia Mbunge maji hayana mbadala na nilikwishafika katika Jimbo lake na kuna fedha ambayo tuliikuta, nawaagiza sasa DDCA wafike haraka katika kuhakikisha wanakichimba kisima kile ili wananchi wake waweze kupata huduma ya maji ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved