Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Yosepher Ferdinand Komba

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. YOSEPHER F. KOMBA aliuliza:- Katika Kijiji cha Sakale, Kitongoji cha Kwempasi, Tarafa ya Amani katika Wilaya ya Muheza wananchi waligundua uwepo wa madini na shughuli za uchimbaji zilianza, lakini baada ya muda Serikali imefunga machimbo yale:- Je, ni lini Serikali itaandaa utaratibu wa kufungua machimbo hayo ili wachimbaji wadogo hususan vijana wazawa waweze kunufaika.

Supplementary Question 1

MHE. YOSEPHER F. KOMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nina maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Waziri ameeleza sababu ya kufungwa kwa eneo hili la madini, naomba nimuulize Mheshimiwa Waziri, ni utaratibu gani ambao wameuandaa baada ya manyanyaso makubwa kwa wananchi, baada ya unyanyasaji mkubwa kunyang’anywa mali kuumizwa, ambao ulitokea kwenye eneo hili la madini. Wao kama Wizara wamechukua hatua gani kwa wananchi wa eneo lile, ambao walipata manyanyaso makubwa baada ya kugundua madini kwenye eneo hili?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Mheshimiwa Waziri atuambie huyo mwekezaji mkubwa au mwekezaji mzawa, wao kama Wizara wameshamtafuta au wameshampata au wameshatangaza au ni lini atapatikana ili aanze uchimbaji ili wananchi wanaozunguka eneo lile waweze kunufaika nalo? Ahsante.

Name

Doto Mashaka Biteko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukombe

Answer

WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la Mheshimiwa Yosepher kama ifuatavyo; kwanza hili la manyanyaso kama lipo na lilifanyika na watu walinyang’anywa mali zao ni muhimu tu tukatumia vyombo vyetu tulivyonavyo vya usalama kupitia Jeshi la Polisi malalamiko haya yaweze kuwasilishwa ili hatua ziweze kuchukuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili je, tumetafuta muwekezaji naomba tu nimpe taarifa kwamba watanzania wengi sana ambao wameomba kuchimba kwenye maeneo hayo na nieleze tu kwamba Mheshimiwa Adadi tulienda pale SAkale tukafanya mkutano kwa wananchi na kwa watu ambao walionesha nia ya kuwekeza tumewapa taratibu za kufuata kwa sababu kwa kweli kuchimba pale ni kwenye mto ni lazima tuzingatie sheria ili tusije tukaharibu chanzo cha maji, kwa hiyo wako wengi tumewapa taratibu za kufuata ili waweze kuchimba kwa mujibu wa sheria.