Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mary Deo Muro

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARY D. MURO aliuliza:- Viwanja vya Mwanalugali Mjini Kibaha vimeshindwa kupimwa kutokana na mgogoro uliopo kwa wenye ardhi hiyo kutolipwa fidia wakati wa upimaji mwaka 2000:- Je, Serikali inatoa msaada gani kwa wananchi hao ambao wameshindwa kuendeleza maeneo yao na kuwasababishia umaskini mkubwa?

Supplementary Question 1

MHE. MARY D. MURO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa kuwa ni miaka 19 tangu mgogoro uanze na wananchi wale hawafanyi mwendelezo wowote, walijenga majengo yao wakasimamishwa. Je, Serikali ipo tayari kuwalipa fidia ya hasara ambayo wameipata kwa muda wote huo?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la mama yangu Mheshimiwa Mary Muro, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli ni muda mrefu na kwenye taarifa yangu hapa nimesema. Hata hivyo, kila kitu lazima kina win-win situation na ndiyo maana nimesema kwamba kuna mkakati unaendelea. Kikubwa zaidi nimuelekeze Mkurugenzi wetu wa Halmashauri ya Kibaha aende akakae na wananchi wakubaliane nini kifanyike kwa ajili ya eneo hilo ili kuondoa mgogoro huu ambao umedumu kwa muda mrefu lakini mwisho wa siku kila mwananchi awe na furaha.

Kwa hiyo, Mheshimiwa mama Muro achukue maelekezo yangu haya kwamba namuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri yetu aende kukaa na wananchi pamoja na timu yote na ikiwezekana Kamati ya Fedha, on site meeting, wakubaliane nini kifanyike ili mradi kuondoa dukuduku za aina yoyote kwa wananchi wetu wa Kibaha Vijijini.