Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Saada Salum Mkuya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Welezo

Primary Question

MHE. SAADA MKUYA SALUM aliuliza:- Kumekuwa na vitendo vya mauaji ya mara kwa mara kwa upande wa Zanzibar katika siku za hivi karibuni; mauaji hayo yanatokana na aidha kuuwawa kwa wanaoshukiwa kuwa ni wezi au mauaji mengine hayajulikani chanzo chake. (a) Je, Serikali imeshafanya tathmini ya hali hiyo? (b) Je, ni washukiwa wangapi kwa kipindi cha karibuni ambao wametiwa hatiani kutokana na vitendo vya mauaji kwa upande wa Zanzibar?

Supplementary Question 1

MHE. SAADA MKUYA SALUM: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, naishukuru Serikali, namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu mazuri kabisa hata hivyo nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, inaonekana kwamba utaratibu huu wa utoaji wa elimu hauko effective na ndiyo maana haya matukio yameendelea kwa kiasi hicho ambacho Mheshimiwa Waziri amekitaja.

Je, Serikali haioni kama kuna umuhimu wa kubadilisha utaratibu wa utoaji wa elimu kwa wananchi ili wasiendelee kuchukua sheria katika mikono yao?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, inawezekana kabisa yanatokea haya mauaji kwa sababu wananchi wenyewe wanakuwa wanakosa imani na jeshi la polisi na kwamba pengine wale watuhumiwa wakipelekwa katika vituo vyetu vya polisi, kesho yake wanawaona wako mitaani. Kwa hivyo, Serikali ina mkakati gani wa kuliondoa hili miongoni mwa jamii ili kuona kwamba haki inatendeka kwa kila ambaye amefanya kosa na wale ambao hawajafanya makosa? (Makofi)

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Sasa nijibu maswali yake mawili ya nyongeza kama ifuatavyo; kuhusiana na utaratibu ambao tunatumia nadhani siyo utaratibu mbaya, hata hivyo tunachukua mapendekezo yake kama ni changamoto ili tuangalie jinsi gani tunaweza tukfikia zaidi wananchi waweze kupata taarifa. Hata hivyo nimthibitishie Mheshimiwa Mbunge kwamba wananchi kwa kiasi kikubwa wana imani na jeshi lao la polisi na kutokana na amani na utulivu na upungufu wa takwimu za uhalifu nchini ambao unaendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nikiri kwamba kwa wale wananchi ambao wanakosa imani na baadhi ya askari polisi wachache ambao pengine wamekuwa wakitekeleza majukumu yao kinyume na maadili, niwahakikishie wananchi kwamba wakati wote tunavyobaini askari wa aina hiyo tumekuwa tukichukua hatua stahiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo bahati njema ni kwamba askari hao ni wachache, walio wengi wanafanya kazi zao vizuri kwa uadilifu na ndiyo maana nchi yetu inaendelea kuwa salama mpaka sasa hivi.