Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Machano Othman Said

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. MACHANO OTHMAN SAID (K.n.y. MHE. JAKU HASHIM AYOUB) aliuliza:- (a) Je, ni lini TRA itakaa na wafanyabiashara wa Tanzania kusikiliza vilio vyao licha ya kila Mkoa unayo Ofisi ya TRA? (b) Je, ni sababu gani zinazofanya mizigo inayotoka Zambia, Uganda, Kenya, DRC haipati usumbufu inapoingia Jijini Dar es Salaam katika bandari lakini mizigo kutoka Zanzibar inakuwa kero kubwa inapoingia Jiji la Dar es Salaam kupitia bandarini? (c) Je, ni lini TRA itaweka Ofisi kila Mkoa kusikiliza kero za wafanyabiashara ambao wanahisi wanaonewa na vilevile kuweka Mwanasheria kila Ofisi ili pasiwepo na manung’uniko ya wafanyabishara kuonewa?

Supplementary Question 1

MHE. MACHANO OTHMAN SAID: Mheshimiwa Spika, nakushukuru na pia nimshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake. Pamoja na majibu yake, naomba kuuliza swali moja la nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa wananchi wengi wa Zanzibar shughuli zao ni uvuvi; na kwa kuwa biashara ya dagaa ni kubwa sana kwa Zanzibar na soko lake kubwa ni Congo (DRC) na Rwanda. Ni sababu gani inasababisha kila tani moja ya dagaa kutozwa dola 400 katika mpaka wa Tunduma?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Machano, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nimemsikia vyema amezungumzia na kutaka kujua juu ya mgogoro wa usafirishaji wa mazao ya uvuvi (dagaa) kutoka Tanzania aidha Visiwani na Bara kwenda nje ya nchi na inaonekana tozo ni kubwa na wafanyabiashara kuishindwa kulipa tozo hiyo.

Mheshimiwa Spika, hapa karibuni Wizara yetu ya Mifugo na Uvuvi tulifanya mabadiliko ya tozo mbalimbali za mazao yetu ya mifugo na uvuvi. Tozo zile tulizoziweka zimepelekea wafanyabiashara hasa wa Ukanda wa Pwani kuwa juu ya uwezo wao. Baada ya malalamiko makubwa, Wizara imeyapokea malalamiko yao, imeyafanyia kazi na tumefanya marekebisho ya tozo zile. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya bajeti ya Wizara ya Fedha na tozo mpya kupitishwa na Serikali na kutangazwa katika Gazeti la Serikali, kuanzia tarehe 1 Julai, tunayo matumaini kwamba tozo zile zitashuka sana na wafanyabiashara wataendelea kutoa mazao yale ya mifugo kupeleka katika nchi zingine zinazohitaji. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Mbunge na wafanyabiashara wote wawe na subra muda si mrefu majibu ya jambo hili yatakuwa yamepatikana.

Name

Khatib Said Haji

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Konde

Primary Question

MHE. MACHANO OTHMAN SAID (K.n.y. MHE. JAKU HASHIM AYOUB) aliuliza:- (a) Je, ni lini TRA itakaa na wafanyabiashara wa Tanzania kusikiliza vilio vyao licha ya kila Mkoa unayo Ofisi ya TRA? (b) Je, ni sababu gani zinazofanya mizigo inayotoka Zambia, Uganda, Kenya, DRC haipati usumbufu inapoingia Jijini Dar es Salaam katika bandari lakini mizigo kutoka Zanzibar inakuwa kero kubwa inapoingia Jiji la Dar es Salaam kupitia bandarini? (c) Je, ni lini TRA itaweka Ofisi kila Mkoa kusikiliza kero za wafanyabiashara ambao wanahisi wanaonewa na vilevile kuweka Mwanasheria kila Ofisi ili pasiwepo na manung’uniko ya wafanyabishara kuonewa?

Supplementary Question 2

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Napenda nimuulize Mheshimiwa Waziri, umekuwepo utaratibu wa Waafrika wote, kutoka nchi mbalimbali wanapotaka kuja ndani ya Tanzania na usafiri wao binafsi wanaingia kwa kupata permit katika mipaka yetu. Je, ni kwa nini Wazanzibar ambao wanataka kuingia na magari yao Tanzania Bara kwa ajili ya matumizi na kurudi Zanzibar, hawapati ruhusa hiyo na badala yake wamekuwa wanawekewa vikwanzo kuingia na magari yao kwa matumizi binafsi na baadaye kurudi nayo Zanzibar?

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali moja la Mheshimiwa Khatib, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, amesema vizuri Mheshimiwa Khatib lakini angetusaidia pia kama hata yeye wakati ameingia Tanzania Bara na gari lake alipewa permit kwa ajili ya kuendesha gari lake hilo huku Tanzania Bara?

Mheshimiwa Spika, niliambie Bunge lako Tukufu kwa nini tuko katika mkanganyiko huo. Siku zote naposimama hapa nimekuwa nikisema kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania Bara na Mamlaka ya Mapato Tanzania Visiwani wanatumia mifumo tofauti ya uthaminishaji wa mizigo. Ndiyo maana magari yanapopita Zanzibar kuja huku Tanzania Bara lazima yafanyiwe uthamini upya ili kujiridhisha na kodi ambayo imelipwa ili kuleta fair competition kwenye biashara zetu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hilo linafahamika vizuri na nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kutoka Zanzibar wengi wao katika hili hawakubaliani. Kwa hiyo, niombe tuweze kukubaliana kwenye jambo hili ili tuondoke kwenye mkanganyiko huu na tuweze kuwahudumia watu wetu vizuri.

Name

Frank George Mwakajoka

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Tunduma

Primary Question

MHE. MACHANO OTHMAN SAID (K.n.y. MHE. JAKU HASHIM AYOUB) aliuliza:- (a) Je, ni lini TRA itakaa na wafanyabiashara wa Tanzania kusikiliza vilio vyao licha ya kila Mkoa unayo Ofisi ya TRA? (b) Je, ni sababu gani zinazofanya mizigo inayotoka Zambia, Uganda, Kenya, DRC haipati usumbufu inapoingia Jijini Dar es Salaam katika bandari lakini mizigo kutoka Zanzibar inakuwa kero kubwa inapoingia Jiji la Dar es Salaam kupitia bandarini? (c) Je, ni lini TRA itaweka Ofisi kila Mkoa kusikiliza kero za wafanyabiashara ambao wanahisi wanaonewa na vilevile kuweka Mwanasheria kila Ofisi ili pasiwepo na manung’uniko ya wafanyabishara kuonewa?

Supplementary Question 3

MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii niweze kuuliza swali la nyongeza, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nakumbuka mwaka 2017/2018 Serikali ilitenga karibuni bilioni 900 kwa ajili ya shughuli za maendeleo kwenye Wizara ya fedha, na fedha hizi, zilikuwa zinakwenda kutoa elimu kwa walipa kodi watanzania, na sasa hivi kumekuwa na kero kubwa sana ya kodi kwenye nchi hii, na biashara nyingi zinafungwa katika Taifa hili.

Mheshimiwa Spika, Je, Serikali imejipanga namna gani, namna ya kutoa elimu kwa walipa kodi ili Watanzania hawa waweze kujua wanalipa kodi kutoka kwenye faida, au wanalipa kodi kutoka kwenye mtaji? Kwa sababu elimu hiyo hawana mpaka sasa hivi, ahsante sana. (Makofi)

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, kwenye jibu langu la msingi, nimeelezea Elimu ya Kodi hutolewa katika ngazi mbalimbali, kuanzia ngazi ya Taifa Mamlaka ya Mapato Tanzania hukaa na Wafanyabiashara kuwapa Elimu ya Kikodi physically yaani uso kwa uso lakini pia kupitia Vyombo mbalimbali vya Habari.

Mheshimiwa Spika, lakini pia hata sisi Viongozi Wakuu wa Wizara ya Fedha tumekuwa tukizunguka katika Mikoa mbalimbali kukutana na wafanyabiashara na kupeana Elimu ya Kikodi tukiwa na Wataalamu wetu wa Kikodi. Lakini pia kila mwezi Wakuu wa Mikoa huwa na Mabaraza ya Biashara kwenye Mikoa yao, hukutana na wafanyabiasha na kutoa Elimu ya Kikodi Wataalamu wetu wa Kikodi wanakuwepo.

Vilevile Wakuu wa Wilaya wana Mabaraza ya Biashara ya Wilaya ambapo hukutana na wafanyabiashara, wataalam wetu wa Kodi wakiwepo na Elimu ya Kikodi hutolewa.

Mheshimiwa Spika, nitoe wito kwa Watanzania, kwa Wafanyabiashara wote kuchukua jukumu la kuhudhuria Mikutano hii ili waweze kupata Elimu ya Kikodi na kero zao mbalimbali za Kikodi ziweze kutatuliwa.

Mheshimiwa Spika, lakini Mheshimiwa Mwakajoka amesema biashara nyingi zimefungwa, hili ni suala ambalo linaongelewa katika ujumla wake, nilishaliambia Bunge lako Tukufu kufungwa na kufunguliwa kwa Biashara ni jambo la kawaida katika Mataifa yote Duniani, siyo kwa Tanzania peke yake, na nilishaeleza, rate ya Biashara kufungwa ni ndogo kuliko rate ya Biashara zinazofunguliwa, nashukuru sana.

Name

Rukia Ahmed Kassim

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MACHANO OTHMAN SAID (K.n.y. MHE. JAKU HASHIM AYOUB) aliuliza:- (a) Je, ni lini TRA itakaa na wafanyabiashara wa Tanzania kusikiliza vilio vyao licha ya kila Mkoa unayo Ofisi ya TRA? (b) Je, ni sababu gani zinazofanya mizigo inayotoka Zambia, Uganda, Kenya, DRC haipati usumbufu inapoingia Jijini Dar es Salaam katika bandari lakini mizigo kutoka Zanzibar inakuwa kero kubwa inapoingia Jiji la Dar es Salaam kupitia bandarini? (c) Je, ni lini TRA itaweka Ofisi kila Mkoa kusikiliza kero za wafanyabiashara ambao wanahisi wanaonewa na vilevile kuweka Mwanasheria kila Ofisi ili pasiwepo na manung’uniko ya wafanyabishara kuonewa?

Supplementary Question 4

MHE. RUKIA AHMED KASSIM: Mheshimiwa Spika, ahsante, nami kunipa nafasi ya kuweza kumuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha swali la nyongeza, nilitaka kujua kwa sababu Mbunge ana haki ya kuleta gari yake kwa kupitia exemption kama Mbunge, ana haki ya kuileta Tanzania Bara au Tanzania Visiwani. Ni kwani basi anapoleta gari yake Tanzania Visiwani, akiileta Bara hawezi kupewa namba ya hapa mpaka anaambiwa ailipie difference? (Makofi)

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, nimeshaeleza changamoto ya Kimfumo tuliyonayo, unapopewa namba ya Tanzania Bara, maana yake gari ile inasajiliwa kutumika Tanzania Bara, kwa hiyo, kama inasajiliwa kutumika Tanzania Bara na utofauti wa Kimfumo nilioueleza ni lazima tuweze kuthaminisha gari yako sasa inasajiliwa Tanzania Bara tukupe namba ya Tanzania Bara na uweze kulipia utofauti ule wa Kodi uliopo kwa sababu ya mfumo wetu wa utofauti kati ya Mamlaka mbili hizi ili gari lako liweze kutumika Tanzania Bara.