Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Flatei Gregory Massay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Vijijini
Primary Question
MHE. FLATEI G. MASSAY (K.n.y. MHE. MARTHA J. UMBULLA) aliuliza:- Ujenzi wa senta ya Michezo ya riadha katika Mkoa wa Manyara hususani Wilaya ya Mbulu imekuwa ni kilio cha muda mrefu kwa viongozi na wananchi wa eneo husika kutokana na vijana wengi kuwa na vipaji katika mchezo wa riadha na michezo mingine:- (a) Je, ni lini Serikali itasikiliza kilio cha muda mrefu na kujenga senta ya michezo ya riadha Mkoani Manyara ili vijana wengi wenye vipaji waweze kunufaika? (b) Je, Serikali haioni kuwa kwa kujenga senta ya michezo Manyara itaweza kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana wa Mkoa huo na maeneo jirani kama Singida, Arusha na Dodoma ambako kuna vipaji hivyo?
Supplementary Question 1
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza, kwa kuwa Mbulu walishapewa ahadi ya kujengewa uwanja na Olympic na sasa wale wameondoka na eneo hilo lipo mpaka sasa na wananchi wa Mbulu wamekubali kutoa eneo hilo. Je, Serikali haioni ndiyo sasa wakati wa kuja kuwekeza au kujenga kituo hicho Mbulu?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa wanariadha wazuri ambao wamevunja rekodi ya dunia mpaka leo na haijawahi kuvunjwa mfano Philbert Bai ambao wamekuwa msaada mkubwa kwa Tanzania, je, Serikali haioni sasa ndiyo muda muafaka wa kujenga kituo hicho Mbulu kwa sababu uwezo wa Mbulu na uoto wa asili na hali ya hewa inawaruhusu wanariadha kuweza kufanya mazoezi na kushinda Olympic?
Name
Nape Moses Nnauye
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtama
Answer
WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza Serikali inatambua kazi nzuri iliyofanywa na wanariadha wanaotoka Mbulu wakiwemo akina Philbert Bai na wenzake. Tunakubaliana na hoja kwamba kama eneo lipo ambalo kwa kweli halitahitaji fidia na litaondoa hii haja ya mazungumzo ya kupata eneo, tutashauriana na Serikali ya Mkoa wa Manyara kuona namna ambavyo tunaweza kulitumia eneo hilo kwa ajili ya kujenga kituo hiki.
Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana naye kwamba kwa kutambua mchango wa wanariadha kutoka Mbulu na namna nzuri ya kuwaenzi nadhani ni vizuri tukaangalia namna ya kujenga kituo hiki Mbulu kwa kuzingatia mazingira hayo.
Name
Susan Anselm Jerome Lyimo
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FLATEI G. MASSAY (K.n.y. MHE. MARTHA J. UMBULLA) aliuliza:- Ujenzi wa senta ya Michezo ya riadha katika Mkoa wa Manyara hususani Wilaya ya Mbulu imekuwa ni kilio cha muda mrefu kwa viongozi na wananchi wa eneo husika kutokana na vijana wengi kuwa na vipaji katika mchezo wa riadha na michezo mingine:- (a) Je, ni lini Serikali itasikiliza kilio cha muda mrefu na kujenga senta ya michezo ya riadha Mkoani Manyara ili vijana wengi wenye vipaji waweze kunufaika? (b) Je, Serikali haioni kuwa kwa kujenga senta ya michezo Manyara itaweza kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana wa Mkoa huo na maeneo jirani kama Singida, Arusha na Dodoma ambako kuna vipaji hivyo?
Supplementary Question 2
MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Kuna msemo wa Kiswahili unaosema samaki mkunje angali mbichi. Ujenzi wa kituo hicho hautakuwa na maana kama hatujawekeza huku chini. Tunatambua kwamba wakati Serikali inapanua elimu walihakikisha kabisa viwanja katika shule zetu za msingi havipo kwa maana kwamba walijenga shule za pili. Je, Serikali inasema nini kuhakikisha kwamba shule zetu za msingi zina viwanja ili watoto waanze kucheza riadha au michezo mingine ili sasa hivi vituo wanavyovijenga huku juu viwe na maana?
Name
Nape Moses Nnauye
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtama
Answer
WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza siyo kweli kwamba Serikali ilihakikisha kwamba shule hizi hazina viwanja. Bahati mbaya iliyotokea yako baadhi ya maeneo ambapo suala la kutenga viwanja vya kutosha halikuzingatiwa wakati wanapanga mipango na maeneo mengine viwanja vilichukuliwa vikabadilishwa matumizi.
Mheshimiwa Naibu Spika, tumeendelea kusisitiza kwanza katika kila mpango wa ardhi kuhakikisha tunatenga maeneo ya michezo siyo tu kwenye shule, lakini maeneo ya michezo yatengwe kwenye makazi ya watu ili kurahisisha watu kushiriki michezo kwenye maeneo yao ya makazi. Pili, tumeendelea kukagua na kurudisha maeneo ambayo yamevamiwa na kubadilishwa matumizi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini Waheshimiwa Wabunge ninyi ni Madiwani tusaidieni mambo mawili. La kwanza, hakikisheni hakuna mipango ya matumizi ya ardhi inapitishwa wakati hakuna maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya michezo.
Pili, shule hizi zinaendeshwa na kumilikiwa na halmashauri zetu. Sisi Waheshimiwa Wabunge ambao ni Madiwani tukiwa wakali kwenye kubadilisha matumizi ya maeneo yetu bila shaka viwanja vitapatikana na michezo yetu itaendelea. Nakubaliana na wewe michezo ili iendelee lazima ianze ngazi ya chini, habari ya kuanzia ngazi ya juu tutapoteza muda wetu bure.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved