Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Innocent Sebba Bilakwate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyerwa

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza:- Eneo la Rubwera Kata ya Kyerwa ndiyo Makao Makuu ya Wilaya na maeneo mengi yalikuwa ya wananchi, kuna eneo lilichukuliwa na Jeshi la Magereza na wananchi walizuiliwa kufanya shughuli yoyote kwenye eneo hilo. Je, ni lini Serikali itawalipa fidia wananchi hawa kama walivyoahidiwa?

Supplementary Question 1

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwanza nisikitike sana kwa majibu ambayo yametolewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, uthaminishaji wa maeneo yale umefanyika zaidi ya miakakaribia miaka minne, na kwa mujibu wa sheria inabidi warudi tena kufanya uthaminishaji upya.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kama wameshindwa huu wa kwanza kulipa, watawezaje kufanya uthaminishaji wa awamu ya pili? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, je, mko tayari kuwatangazia wananchi wa Rwenkorongo pale Kyerwa kuwa mmeshindwa kuwalipa ili waweze kuendeleza maeneo yao? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa sababu inaonesha moja kwa moja mmeshindwa kuwalipa wananchi, mko tayari kuongea na Halmashauri ili iwatafutie maeneo mengine ambayo hayatahitaji fidia? (Makofi)

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali haijashindwa kulipa fidia wananchi na Serikali ina nia ya kulipa fidia wananchi. Kama ambavyo nimezungumza katika majibu yangu ya msingi, ni kwamba fidia hizi, maeneo haya ni mengi ambayo yanahitaji kulipwa fidia na suala hili haliwezi likafanyika kwa wakati mmoja.

Kwa hiyo, ninalirudia jibu langu la msingi ambalo nimejibu kwamba fidia za eneo hili ambalo lilichukuliwa kwa ajili ya magereza na maeneo mengine, najua kuna Waheshimiwa Wabunge ambao maeneo yao mengine vilevile yanahitaji kulipwa fidia, zitalipwa kwa awamu kadri hali ya kifedha na kibajeti itakavyoruhusu.