Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Victor Kilasile Mwambalaswa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lupa

Primary Question

MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA (K.n.y. MHE. MARTHA M. MLATA) aliuliza:- Je, ni lini Serikali itajenga vizuri barabara za Kibaya - Urughu, Urughu – Mtekente na Mtekente – Ndago zilizopo Wilayani Iramba ili kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo?

Supplementary Question 1

MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa Serikali kuvifanyia matengenezo barabara zote ambazo zimeulizwa kwenye swali hili, lakini kwa mwaka huu wa fedha 2018/2019, barabara ya Kibaya Urughu imeharibika sana kwa sababu ya mvua, je, Serikali inasema nini kuhusu matengenezo ya barabara hiyo?

Mheshimiwa Spika, Swali la pili barabara zilizopo katika Jimbo la Mheshimiwa Mlata Singida zinafanana sana na barabara za Wilaya ya Chunya, bahati mbaya kwa miaka miwili mfululizo huko Chunya, TARURA hawajafanya kazi yoyote kuzitengeneza barabara za vijijini, hasa hasa barabara ya kutoka Chunya kwenda Soweto; Isenyela kwenda Sangambi; Kiwanja kwenda Ifumbo; Chunya kwenda Mapogolo; Lupa kwenda Lualaje; Chunya kwenda Sangambi, lakini kubwa kuliko zote barabara ya kutoka Sangambi kwenda Chunya ni mahandaki haipitiki kabisa, je, Serikali inasema nini kuhusu matengenezo ya barabara hiyo?

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Spika, katika swali lake la kwanza anaongelea eneo la Urughu ambalo barabara imeharibika kutokana na mvua nyingi ambazo zimenyesha, ni ukweli usiopingika kwamba pale ambapo mvua zinanyesha nyingi na hasa katika barabara ambazo zinatengenezwa kwa kiwango cha vumbi ni uhakika kwamba kunakuwa na uharibifu mkubwa.

Mheshimiwa Spika, ni vizuri tukawasiliana na Mheshimiwa Mbunge ili tukajua ukubwa wa tatizo ili tuweze kutoa maelekezo kwa TARURA ili matengenezo ya dharura yaweze kufanyika ili barabara hii iendelee kupitika kipindi chote, wananchi waendelee kupata huduma na kufanya shughuli zao za kiuchumi.

Mheshimiwa Spika, lakini anaongelea katika jimbo lake ambalo anasema linafanana sana na swali la msingi na anaeleza kwamba katika jimbo lake TARURA haijafanya kazi yoyote kwa mwaka mzima. Hali kama hii hatujaipata pahali pengine popote, ni vizuri tukawasiliana na Mheshimiwa Mbunge tukajua hasa nini ambacho kimetokea hadi barabara isitengenezwe na hali bajeti imekuwa ikitengwa.

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Primary Question

MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA (K.n.y. MHE. MARTHA M. MLATA) aliuliza:- Je, ni lini Serikali itajenga vizuri barabara za Kibaya - Urughu, Urughu – Mtekente na Mtekente – Ndago zilizopo Wilayani Iramba ili kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo?

Supplementary Question 2

MHE. MWIGULU L. NCHEMBA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Kibaya, Urughu - Mtekente - Mtowa na Sheluwi ni moja ya barabara inayobeba uchumi wa Iramba na katikati ya Mtekente na Mtowa pana daraja la kisasa sana limejengwa.

Je, kwa nini Wizara ya Ujenzi isiipandishe barabara hii kufuatana na umuhimu wake ili iwe chini ya TANROADS iweze kujengwa kwa kisasa na iweze kusaidia wananchi hawa?

Name

Elias John Kwandikwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Spika, ni kweli Waheshimiwa Wabunge watakubaliana na mimi kwamba tumekuwa na chombo hiki TARURA na dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kwamba TARURA inafanya kazi nzuri na kweli nitumie nafasi hii niwapongeze TARURA kwa sababu wameanza vizuri maeneo mengi, wanafanya vizuri na kumekuwa na mchakato wa kuzitambua barabara zetu kwa nia dhabiti ya kuweza kuziboresha.

Mheshimiwa Spika, nimuombe Mheshimiwa Mbunge kwamba utaratibu wa kupandisha barabara uko kisheria na kama saa nyingine itapendeza watumie nafasi hiyo kwa vikao walivyonavyo ili waweze kuleta mapendekezo na sisi kama Serikali tutazama kwa namna hiyo kwa mujibu wa taratibu zilizokuwepo ili kama itakidhi kupandishwa basi Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana atafanya hivyo. Lakini kimsingi ni kwamba TARURA ipo kwa ajili ya kuboresha barabara zetu na nifahamishe tu kwamba itaenda kujenga barabara zetu mpaka kiwango cha lami.

Name

Joyce Bitta Sokombi

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA (K.n.y. MHE. MARTHA M. MLATA) aliuliza:- Je, ni lini Serikali itajenga vizuri barabara za Kibaya - Urughu, Urughu – Mtekente na Mtekente – Ndago zilizopo Wilayani Iramba ili kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo?

Supplementary Question 3

MHE. JOYCE B. SOKOMBI: Mheshimiwa Spika, tatizo lililoko Iramba halina tofauti na tatizo lililoko katika Mkoa wa Mara hasa barabara ya Musoma - Busekela ambayo ilitengewa kilometa 42 lakini cha ajabu barabara hii iliyojengwa ni kilometa tano tu. Ninachotaka kujua hizi kilometa 37 zitajengwa lini? Ahsante.

Name

Elias John Kwandikwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba kwa kutambua umuhimu wa barabara hii anayozungumza Mheshimiwa Mbunge tumeanza kufanya ujenzi wa kilometa tano na hii tunazingatia kwamba yale maeneo ambayo ni korofi tunaanza kuyawekea lami na hivyo hivyo maeneo yote nchi nzima kwamba tunapokuwa na utaratibu wa kujenga barabara zetu yale maeneo ambayo tunaona kwamba ni muhimu tuyaboreshe tunaanza kufanya hivyo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kwanza nimuombe Mheshimiwa Mbunge aridhike kwamba tumeanza kuchukua hatua nzuri ili kufanya ujenzi kwenye maeneo ambayo tunaona kwamba ilikuwa ni muhimu tuyaboeshe na tutaendelea kufanya hivyo. Tukipata fedha za kutosha tutakwenda kujenga barabara hii yote, kwa hiyo, uvute subira hatua ndio hivyo tumeanza kidogo lakini kadri tunavyopata fedha tutakwenda kuiboresha barabara hii na tutaendelea kuboresha maeneo yote ambayo yanaleta usumbufu kwa wananchi wakati wanasubiri barabara ya lami yote ijengwe basi waweze kupita na kufanya shughuli zao za maendeleo, ahsante sana.