Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Leah Jeremiah Komanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Meatu

Primary Question

MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza:- Serikali ina Mkakati gani wa kuhakikisha kuwa watumishi hewa hawapo katika payroll ya Serikali:- Je, Serikali inadhibiti vipi mishahara ya watumishi wasiostahili kulipwa kama wastaafu, waliofariki, walioacha kazi na waliofukuzwa kazi katika Halmashauri?

Supplementary Question 1

MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu ya Serikali, bado malipo ya mishahara na makato kwa watu ambao sio Watumishi wa Umma bado yanaendelea kulipwa kulingana na hoja za Mkaguzi CAG. Kwa mfano 2017/2018 shilingi milioni 207.3 zililipwa. Je, ni kwa nini Wizara ya Fedha inachelewa kukamata yaani ku-hold makato yaliyolipwa kwa Taasisi mbalimbali na kusimamisha makato ya mishahara kwa kiwango sawa na watumishi wasiostahili kulipwa? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; je, Serikali inachukua baada ya muda gani kuweza kuhuisha taarifa za watumishi ili waweze kushughulikiwa haraka kwa kuondolewa katika Mfumo wa Malipo ya Mishahara? (Makofi)

Name

Dr. Mary Machuche Mwanjelwa

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mbeya Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UTUMISHI NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba nami nijibu maswali mawili madogo ya nyongeza ya Mheshimiwa Leah Komanya kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kama Serikali tulifanya HR Audit kwa Watumishi wote wa Umma wakiwepo na hawa wa TAMISEMI zaidi ya 197,000 mwaka ule wa 2016, lakini watumishi wote wale wanaoacha kazi, waliofukuzwa kazi, waliofariki, hawasalii kabisa kwenye Payroll ya Serikali. Naomba niliambie Bunge lako Tukufu na Watanzania wote kwamba kama Serikali sasa hivi tumeboresha Mfumo wa Utumishi na Mishahara kiasi cha kwamba hatutatumia tena ile Lawson Version 9 ambayo tulikuwa tunatumia, tuna Mfumo wetu wenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, taarifa zozote zinazotoka kwa waajiri wote, kama ziko sahihi zinatolewa siku hiyo hiyo ikiwepo pamoja na malipo ya madai yote. Kwa hiyo, nawataka waajiri wote nchini kuhakikisha kwamba wanatuletea taarifa ambazo ni sahihi na kwa wakati na kutokana na mfumo wetu huu mpya ambao tunauanza mwezi ujao, basi taarifa za watumishi wote zitatolewa siku hiyo hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. (Makofi)