Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Eng. James Fransis Mbatia

Sex

Male

Party

NCCR-Mageuzi

Constituent

Vunjo

Primary Question

MHE. JAMES F. MBATIA (K.n.y. MHE. JOHN J. MNYIKA) aliuliza:- Pamoja na kuwa karibu na Makao Makuu ya TANESCO, baadhi ya maeneo ya Jimbo la Kibamba hayana umeme na yale yenye umeme kiwango chake hupungua na kuongezeka (low voltage and fluctuation):- (a) Je, Serikali inaweza kuwasilisha orodha ya maeneo yasiyo na umeme katika Kata za Saranga, Mbezi, Msigani, Goba , Kwembe na Kibamba, na lini maeneo hayo yatapatiwa umeme; (TANESCO)? (b) Je, Serikali ina inachukua hatua gani kuondoa tatizo la kupungua na kuongezeka kwa umeme katika Kata hizo?

Supplementary Question 1

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Kwa kuwa lengo la saba la Maendeleo Endelevu ya Duniani ni kuwa na umeme nafuu wa uhakika, endelevu na wa kisasa kwa wananchi wote; na kwa kuwa sekta ya nishati ni sekta nyeti; uzalishaji wa umeme, usafirishaji wa umeme na usambazaji wa umeme, Serikali imefikia hatua gani ya kuhakikisha uzalishaji na usambazaji unakuwa na ubia; na usafirishaji ukamilikiwa na Serikali ili effectiveness katika upatikanaji wa nishati uweze ukawa kwa wote?
Pili, kwa kuwa Kata zilizotajwa kwenye Jimbo la Kibamba, matatizo yake ni sawa sawa na Kata za Kahe Mashariki, Kahe Magharibi, Njia Panda Makuyuni katika Jimbo Vunjo, je, Serikali haiwezi ikaona kwa kuwa hili ni Bunge jipya, ikaleta mpango kazi wa usambazaji wa umeme kwa Majimbo yote ya uchaguzi nchi nzima ili Wabunge waweze kupata ikawa ni rahisi kufuatilia katika Majimbo yao ya uchaguzi? (Makofi)

Name

Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Musoma Vijijini

Answer

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika, kwanza swali la usambazaji, siyo kwamba tuna mipango, tunayo miradi. Kwa hiyo, kwa sasa tunaongeza usambazaji wa umeme unaotokea Iringa kwenda Dodoma, Dodoma mpaka Mikoa ya Kaskazini Magharibi, tunatoka kwenye kilovoti 220 kwenda kilovoti 400.
Mheshimiwa Spika, nadhani waliosafiri kwenye hiyo barabara wameona nguzo zile za chuma kubwa, halafu tunajenga transmission line kutoka mpakani mwa Zambia kwenda mpaka Namanga, kutoka kilovoti 220 mpaka kilovoti 400. Ni kwa sababu tunaingia kwenye biashara ya kuuziana umeme kama inavyofanyika duniani kote. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ukiwa pale Canada unaangalia wanauzia umeme Marekani Niagara Falls, ukiwa kule Iceland, Polland na nchi zote; kwa hiyo, Tanzania inayokuja ni ya umeme mwingi na wa bei nafuu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sasa nije umeme wa bei nafuu. Ni kwamba kwa sasa hivi ukichukua umeme wote tulionao nchini, hata wa watu binafsi, hatuvuki megawati 1,500; lakini mimi nitachangia siku ya mwisho kuonyesha namna gani tunajenga viwanda vyenye umeme wa bei nafuu.
Mheshimiwa Spika, kama tunataka kuingia nchi ya kipato cha kati miaka 10 ijayo lazima tuwe na Megawati zaidi ya shilingi 10,000/=. Ndiyo maana nakaribisha hata nyie Wabunge kama mnataka kuwekeza kwenye umeme, njooni. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, bei ya umeme, wengine wanasema nilisema bei ishuke, haijashuka. Mheshimiwa Mbatia ni hivi nilisema tunapiga hesabu; hizi bei huwezi ukaongea kwenye majukwaa. Kwa hiyo, mategemeo yangu ni kwamba TANESCO na EWURA wanapiga hesabu, nitakaa nao. Umeme sasa hivi tunauziwa kwa senti 12 kwa unit moja. Tunataka kuushusha bei, lakini siyo kwenye majukwaa. Hesabu inapigwa na tarakimu mtazipata. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile usambazaji wa umeme kwa wakazi wa Dar es Salaam, katikati ya jiji, kwa mara ya kwanza kabisa tunataka kuachana na matatizo ya umeme. Nyaya zote zinapita chini ya ardhi. Ile ya TANESCO kufukuzana na magari kutafuta wapi nyaya zimeharibika tunataka kuachana nayo kuanzia mwezi wa Nne. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, station ile inatizamana na Hospital ya TMJ ambayo itakuwa inaangalia wapi kuna matatizo. Huo mradi nadhani Mkandarasi nimemwambia ikifika mwezi wa nne, mvua sijui miti imeangukia kule katikati ya Dar es Salaam tutaachana nayo.
Ndugu zangu wa Mbagala na Temeke, tunajenga transfoma kubwa sana ambayo itatatua matatizo ya usambazaji. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Jimbo la Mnyika kote tunatoa transfoma ambazo zilikuwa za kVA100, kwenda 200.
Kwa hiyo, miradi ndugu yangu ni mingi sana Mheshimiwa Mbunge, tukileta hapa, mimi nadhani tuonane huko huko, field mnaziona. Ahsante. (Makofi)