Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ussi Salum Pondeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chumbuni

Primary Question

MHE. USSI SALUM PONDEZA AMJADI aliuliza:- Vituo vingi vidogo vya Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja vimefungwa na kuwapa wakati mgumu wananchi wanapohitaji huduma ya polisi wakati vilikuwa vinasaidia kupambana na uhalifu kwa wakati muafaka:- (a) Je, ni kwa sababu gani vituo hivyo vimefungwa na wananchi kulazimika kupata huduma katika vituo vikubwa kinyume na malengo ya kuanzishwa kwake? (b) Je, ni kwa nini vituo vya Kilimani, Mkunazini, Mlandege pamoja na vituo vingine vimefungwa na wananchi kulazimika kufuata huduma umbali mrefu? (c) Je, hatua ya kufunga vituo hivyo inasaidia vipi katika kupambana na uhalilfu hasa katika maeneo ya katikati ya mji wa Zanzibar na Serikali ina mpango gani na majengo yake?

Supplementary Question 1

MHE. USSI SALUM PONDEZA AMJADI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri lakini nina swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, amesema kuna upungufu wa maaskari lakini katika Jimbo langu la Chumbuni tuna matatizo sana ya kupatiwa kituo cha polisi. Kuna kituo kidogo cha Polisi ambacho kinahudumia majimbo zaidi ya manne ya Shaurimoyo, Mwera, Mto Pepo na Chumbuni yenyewe ambao watu wanaoishi pale ni zaidi ya 67,000.

Mheshimiwa Spika, nimekuwa nikiuliza zaidi ya mara saba au nane humu ndani ya Bunge na nimepata ahadi mara nyingi kutoka kwa Mheshimiwa Waziri au Wizara kuwa watafanyia matengenezo au watakiboresha kituo kile kidogo. Je, yupo tayari kuniahidi au kuiahidi hadhara hii kuwa watakijenga kituo kile kwa kushirikiana na Mbunge?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, kwanza nichukue fursa hii kumpongeza kwa dhamira yake ya dhati ya kushiriki katika ukarabati wa kituo hicho. Nimhakikishie kwamba tupo tayari kushirikiana naye kuhakikisha kwamba kituo hiki kinafanyiwa matengenezo ili kiweze kutumika vizuri zaidi.

Name

Flatei Gregory Massay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Vijijini

Primary Question

MHE. USSI SALUM PONDEZA AMJADI aliuliza:- Vituo vingi vidogo vya Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja vimefungwa na kuwapa wakati mgumu wananchi wanapohitaji huduma ya polisi wakati vilikuwa vinasaidia kupambana na uhalifu kwa wakati muafaka:- (a) Je, ni kwa sababu gani vituo hivyo vimefungwa na wananchi kulazimika kupata huduma katika vituo vikubwa kinyume na malengo ya kuanzishwa kwake? (b) Je, ni kwa nini vituo vya Kilimani, Mkunazini, Mlandege pamoja na vituo vingine vimefungwa na wananchi kulazimika kufuata huduma umbali mrefu? (c) Je, hatua ya kufunga vituo hivyo inasaidia vipi katika kupambana na uhalilfu hasa katika maeneo ya katikati ya mji wa Zanzibar na Serikali ina mpango gani na majengo yake?

Supplementary Question 2

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Kituo cha Polisi Yaeda Chini kimejengwa na wananchi mpaka kufikia mwisho, kilichobaki ni nyumba za askari. Je, Serikali ipo tayari kuleta fedha za kujenga nyumba za askari ili kituo hicho kifunguliwe?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Flatei, Mbunge wa Mbulu Vijiji, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Flatei kwa jitihada zake kubwa sana. Niliwahi kwenda huko tukashirikiana naye katika kuhakikisha kwamba tunatatua changamoto hii na ameichukua kwa haraka sana na kuifanyia kazi, amejenga kituo kizuri tu.

Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Flatei kwamba Serikali inazithamini sana jitihada zake na za wananchi wa jimbo hilo na hivyo basi katika mkakati wetu wa nyumba za askari nchi zima, tutakapokuwa tumefanikiwa kupata uwezo basi tutashirikina naye vilevile kutatua tatizo hilo la makazi ya askari ili kituo hicho kiwezi kufanya kazi vizuri zaidi. Ahsante.