Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mwanne Ismail Mchemba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Tabora Mjini

Primary Question

MHE. MWANNE I. MCHEMBA (K.n.y. MHE. SEIF K. GULAMALI) aliuliza:- Wilaya ya Igunga ilipata ufadhili wa Benki ya Dunia wa ujenzi wa Vituo vya Afya vya Simbo, Ziba, Chomachankola na Igurubi ambapo Vituo vya Afya vya Ziba, Chomachankola na Igurubi vimekamilika na vifaa tayari vipo japo majengo na vifaa katika Kituo cha Afya cha Chomachankola na Igurubi bado havijaanza kufanya kazi; Kituo cha Afya cha Simbo bado hakijakamilika na vifaa havipo na Wafadhii walishakabidhi Halmashauri bila kukamilisha ujenzi huo:- Je, Serikali inachukua hatua gani kujua nini kilichojificha juu ya Mradi huo kukabidhiwa bila kukamilika?

Supplementary Question 1

MHE. MWANNE I. MCHEMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nami naomba niulize swali dogo la nyongeza, kwanza nichukue nafasi hii kuipongeza sana Serikali yangu ya Awamu ya Tano kwa kazi nzuri ambayo inafanya kukamilisha Vituo vya Afya ambavyo mimi mwenyewe kama Mjumbe wa Kamati hiyo nimejionea kwa macho yangu mwenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu sasa, kwa kuwa Kituo cha Afya Simbo kimekamilika na bado hakijaanza kazi, je, ni lini sasa hivyo vifaa tiba vitapelekwa haraka sana ili kuwapunguzia adha wagonjwa ambao wanakimbilia kwenda Hospitali ya Private ya Nkinga?

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mchemba, Makamu Mwenyekiti wa Kamati yetu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba uniruhusu nipokee pongezi kwa niaba ya Wizara na yeye mwenyewe amekuwa shuhuda amejionea kwa macho yake, lakini katika swali lake anauliza lini Kituo cha Afya hicho ambacho kimeshakamilika kitaanza kutoa huduma kama ambavyo Serikali imekusudia. Naomba nimtoe mashaka Mheshimiwa Mbunge tayari fedha tumeshalipa MSD na vifaa vinanunuliwa moja kwa moja kutoka mtengenezaji, kwa hiyo wakati wowote vifaa vikishakamilika, lakini pia kumekuwa na changamoto ya Wataalam wa kutoa tiba kwa ajili ya usingizi anesthesia, tayari wamepelekwa Bugando mmoja na mwingine amepelekwa Muhimbili ili vifaa vitakapofika na wataalam waweze kutoa huduma ili wananchi wasihangaike kutembea umbali mrefu. (Makofi)