Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Joseph Michael Mkundi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Primary Question

MHE. JOSESPH M. MKUNDI aliuliza:- Kituo cha Afya Bwisya kimekarabatiwa na kuongezewa miundombinu muhimu kufikia kiwango cha hospitali: Je, kwa nini Serikali isipandishe hadhi kituo hicho na kuwa Hospitali ili kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa wakazi wa visiwa vya Ukerewe?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Spika, pamoja na miundombinu mizuri iliyopo katika Kituo cha Bwisya, kuna upungufu mkubwa wa watumishi pale kituoni na kuathiri utoaji wa huduma.

Mosi, je, ni lini Serikali itapeleka madaktari na wahudumu wengine wa afya Bwisya?

Pili, Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe (Nansio), Vituo vya Afya na Zahanati Jimboni Ukerewe vina upungufu mkubwa wa watumishi (chini ya 50%): Ni lini Serikali itapeleka watumishi wa kutosha na hasa ikizingatiwa ugumu wa jiografia ya visiwa vya Ukerewe?

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, imepata kibali cha kuajiri madaktari 610 na kuwapanga kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini kwa kutoa kipaumbele kwenye maeneo yenye upungufu mkubwa. Hivyo baadhi ya Madaktari hao watapangwa kwenye Vituo vya kutolea huduma za Afya Wilaya ya Ukerewe.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuajiri wataalam wa huduma za Afya kwa awamu kwa kadri ya upatikanaji wa fedha.