Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Sixtus Raphael Mapunda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbinga Mjini
Primary Question
MHE. SIXTUS R. MAPUNDA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itapeleka umeme katika Vijiji vya Mpepai na Lipilipili?
Supplementary Question 1
MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa chanzo cha umeme cha maji cha Tulila kipo katika Kata ya Mpepai na miundombinu yake inapitia katika Kitongoji cha elfu mbili na vijiji vya Kata za Mapendano kuelekea Songea, Serikali haioni umuhimu wa kuvipatia Vijiji vya Kata za Mpepai na Kihungu umeme kwanza kabla ya vijiji vingine hasa ukizingatia vijiji hivyo hulinda na kuitunza miundombinu hiyo na hivyo kuwafanya wananchi wa Mpepai kupata hisia za kuwa wametengwa na kubaguliwa kwenye huduma hiyo ya umeme?
Name
Subira Khamis Mgalu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ni kweli miundombinu ya umeme kutoka katika chanzo cha maji cha Tulila inapita katika Kata za Mpepai na Kihungu. Katika Kata ya Kihungu kuna Vijiji vya Pachasita na Kihungu ambavyo tayari vimeunganishwa na huduma ya umeme. Kijiji kimoja cha Lipembe kitapatiwa umeme kupitia mradi wa REA III unaoendelea.
Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu katika jibu la msingi kuwa kupitia utekelezaji wa mradi wa REA III, Mzunguko wa pili, vijiji vyote vya Kata ya Mpepai ambavyo ni Lipilipili, Luhangai, Mtua, Mpepai na Ruvuma chini vitapatiwa umeme.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved