Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Florent Laurent Kyombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkenge

Primary Question

MHE. FLORENT L. KYOMBO Aliuliza: - Kata za Gera, Ishozi, Ishunju, Kanyigo, Kashenye, Bwanjai, Bugandika, Kitobo, Buyango na Ruzinga katika Jimbo la Nkenge zina shida kubwa ya maji licha ya kwamba zipo kwenye mwambao wa Ziwa Victoria. Je, ni lini Serikali itawafikishia wananchi wa kata hizo maji kutoka Ziwa Victoria kama inavyofanya kwa mikoa mingine inayopata maji kutoka katika ziwa hilo?

Supplementary Question 1

MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali naomba kuongeza maswali ya nongeza mawili kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza niishukuru Serikali kupitia Mheshimiwa Dkt. Magufuli, lakini pia na Waziri wa Wizara ya Maji pamoja na Naibu Waziri kwa usimamizi mzuri wa mradi unaoendelea katika Jimbo la Nkenge wa Kyaka Bunazi wa bilioni 15.1 na Mheshimiwa Naibu Waziri nikushukuru sana juzi ulitoka kule kuangalia maendeleo ya mradi.

Mheshimiwa Spika, mradi huo unahudumia vijiji saba katika Kata za Kyaka na Kasambia lakini kata zingine na vijiji ambavyo vimezunguka mradi huo. Je, ni lini Serikali itaongeza thamani ya mradi ya huo ambao una tenki lenye zaidi ya lita milioni mbili kuzunguka Kata za Nsunga, Mutukula, Bugorora, Bushasha ili thamani ya mradi iweze kuongezwa?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili Wilaya ya Misenye ambayo ni ndani ya Jimbo la Nkenge, ina vyanzo vingi vya maji na vyanzo hivi ni pamoja na Mto Kagera, lakini tuna Mto wa Ngono. Je, ni lini Serikali itaona ni vizuri kutumia vyanzo hivyo vya maji kuweza kupeleka maji katika vijiji ambavyo vinazunguka vyanzo hivyo vya Kata za Kakunyu, Kilimile, Mabale pamoja na Miziro? Nakushukuru.

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, nipende kujibu maswali ya Mheshimiwa Mbunge na niseme kwamba mradi huu mkubwa ambao umeutambua na Mheshimiwa Waziri alifika pale na nikupongeze wewe binafsi kwa namna ambavyo umekuwa ukitoa ushirikiano katika Wizara yetu na nikuhakikishie tu kwamba mradi huu kuongezwa thamani tayari michakato imeanza na wataalam wetu wanafika huko hivi karibuni na kila kitu kitakwenda sawa kama ambavyo uliweza kuongea na Mheshimiwa Waziri alipokuwa ziarani katika jimbo lako.

Mheshimiwa Spika, kuhusu kutumia vyanzo vingine vya maji ili kukidhi na kuondoa shida ya maji katika vijiji vile vingine Mheshimiwa Mbunge nikuahidi tu kwamba tunatarajia kufikia mwezi Juni, tutakuwa tumekamilisha hatua mbalimbali za kuona namna gani tunaibua vyanzo vipya lakini vyanzo vile vilivyoko tunaviboresha na kuona mtandao wa maji unaendelea kutawanyika katika jimbo lako vijiji vyote ambavyo havina maji kwa sasa viweze kupata maji. Ahsante.