Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Fredrick Edwad Lowassa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Monduli
Primary Question
MHE. FREDRICK E. LOWASSA Aliuliza:- Mradi wa maji wa BN 520 una ziada ya lita milioni 100 kwa mujibu wa wataalam na Mheshimiwa Rais alikubali ombi la ziada hiyo kujumuishwa kwenye mradi:- Je, ni lini utekelezaji wa ahadi hiyo utaanza?
Supplementary Question 1
MHE. FREDRICK E. LOWASSA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yako mazuri. Ni kweli kwamba Wananchi wa Jimbo la Monduli wanamwamini sana Mheshimiwa Rais na wanaimani kubwa sana na ahadi yake, lakini ni kweli pia tunaamini uongozi wa Wizara ya Maji ukiongozwa na ndugu yangu Mheshimiwa Juma Awesso, hongereni sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, nina maswali mawili ya nyongeza; tayari Monduli kuna miradi ambayo ipo ya maji lakini inasuasua, tunaomba kauli ya Serikali kuhusu mradi na mpango ambao mmejipanga nao.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, tunaomba kuhakikishiwa usimamizi mzuri juu ya ahadi hii ya Mheshimiwa Rais. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge Lowassa kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa miradi ambayo inasuasua mpango wa Wizara ni kuhakikisha kwamba miradi yote inakamilika kufikia wiki ya maji mwaka huu mwezi Machi na tayari wataalam wetu wanaendelea kufanyia kazi kwa maana ya miradi ambayo imetekelezwa kwa kutengeneza miundombinu lakini maji hayako bombani, tunatarajia kufikia mwezi Machi, Wiki ya Maji miradi hiyo itaanza kutoa maji.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu usimamizi wa ahadi ya Mheshimiwa Rais, wote tunafahamu ahadi ni deni na ahadi hii ni ya Mheshimiwa Rais, naomba nimpe amani Mheshimiwa Mbunge kwamba miradi hii tutakwenda kusimamia na nafahamu alikuwa na ahadi na Mheshimiwa Waziri kwenda jimboni kesho lakini ile safari imeahirishwa kwa sababu ya msiba mkubwa uliotokea pale ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kwa hiyo hali itakapotulia kwenye Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Waziri atakwenda na kuhakikisha usimamizi unafanyika vizuri. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved