Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Primary Question
MHE. DEUS C. SANGU Aliuliza:- Je, ni lini Serikali itatimiza ahadi ya kukabidhi kwa wananchi wa Vijiji vya Msanda, Muungano, Songambele na Sikaungu shamba lililokuwa limechukuliwa na Jeshi la Magereza Mollo Sumbawanga lenye ukubwa wa ekari 495?
Supplementary Question 1
MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, siyo kweli kwamba dai la ekari 495 ni jipya, bali ni ahadi ya Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani mbele ya Mheshimiwa Rais wakati huo alipofanya ziara Mkoa wa Rukwa kwamba watawakabidhi wananchi ekari 495. Lililokuwa linasubiriwa ni kukabidhi kwa maandishi kwa sababu Jeshi la Magereza limekuwa likisema kwamba hatuwezi kufanyia kazi matamko ya wanasiasa mpaka tupewe barua kutoka Wizarani. Ni lini Wizara itawapa barua Jeshi la Magereza ili kukabidhi hizo ekari 495 kwa wananchi?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa tamko hili limepelekea Askari Magereza sasa kuingia kwenye mgogoro mkubwa na wananchi na kuwanyanyasa kwa kuwapiga na mara ya mwisho juzi tu hapa nilikuwa huko Jimboni, mama mmoja (na nikikurushia clip utaona) amepigwa na kugaragazwa kwenye matope. Je, Wizara iko tayari kuunda Tume itakayokuja kuchunguza unyanyasaji unaofanywa na hawa Askari Magereza na watakaobainika kunyanyasa wananchi hatua kali za kisheria zichukuliwe iwe fundisho kwa wengine? (Makofi)
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, kwa ruhusa yako, naomba kujibu maswali ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kwanza tufike wakati tukiri kwamba kuna baadhi ya maeneo bado yana mivutano baina ya wananchi na Kambi za Magereza. Swali kwamba ni lini tutatoa hilo eneo, suala la utoaji wa eneo linahitaji taratibu, siyo suala la kusema tunakwenda na kutoa.
Mheshimiwa Spika, lingine amesema watu wananyanyaswa, wanapigwa, kitu ambacho tunakifanya kupitia Wizara, kwanza tutachunguza, tukiona kwamba kuna Maafisa wetu wa Magereza ambao wanahusika na unyanyasaji huo, hatua kali tutazichukua kupitia Wizara yetu.
Mheshimiwa Spika, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved