Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Rwegasira Mukasa Oscar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Biharamulo Magharibi
Primary Question
MHE. OSCAR R. MUKASA aliuliza:- Wananchi wa Kijiji cha Busiri, Wilayani Biharamulo ni miongoni mwa Watanzania wanaoendesha maisha yao kwa shughuli za uchimbaji mdogo mdogo ambazo zinahitaji kuungwa mkono na Serikali kimkakati. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwaunga mkono wachimbaji wadogo wadogo wa Busiri? Je, Serikali iko tayari kuwatembelea wananchi wa Busiri na kuwaelewesha ni namna gani na ni lini itaanza kutekeleza mkakati huo wa kuwaunga mkono wachimbaji wadogo wadogo?
Supplementary Question 1
MHE. OSCAR R. MUKASA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri lakini nina maswali mawili ya nyongeza.
Moja; eneo la Karukwete lina wachimbaji wadogo na lipo jirani kabisa na Kijiji cha Busiri kinachazungumziwa kwenye swali la msingi. Waziri yupo tayari kulijumuisha kwenye mkakati wa kuwawezesha kielimu na uwezeshaji?
Swali la pili; naomba kujua orodha ya mambo ya kiuwezeshaji yatakayofanyika kwa wananchi wa Karukwete na Busiri na lini tutawenda kuzungumza nao kuwafahamisha? Nashukuru sana.
Name
Dr. Medard Matogolo Kalemani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chato
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana na Mheshimiwa Mukasa kwamba eneo la Karukwete nalo litaongezwa kwenye maeneo ya kufikiriwa kwenye eneo hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jibu langu la pili kwenye orodha ya huduma zitakazotolewa kwa msaada huu ni pamoja na kuwapatia ruzuku wachimbaji wadogo. Mwaka huu kwenye bajeti yetu mtaona tumetenga takribani shilingi milioni tisa za Tanzania pamoja na dola bilioni nne kwa ajili ya kuwawezesha wachimbaji wadogo. Pia tutaendelea kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo ili waweze kuwa na uchimbaji wenye tija.
Pamoja na hayo bado Wizara yetu itatuma wataalam wa GST iyafanyie tathmini maeneo yote yatakayotengwa ili wachimbaji wawe na uhakika wa uchimbaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee kuongeza kwa manufaa ya wengine kwamba maeneo ambayo tutayatenga yapo mengi tunategemea kutenga eneo la Kasubwiya hekta 495, eneo la Nyaluyeye hekta 658, eneo la Matabe hekta 659 na maeneo mengi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tutaendelea kuwawezesha.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved