Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Alfred James Kimea
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Korogwe Mjini
Primary Question
MHE. ALFRED J. KIMEA Aliuliza:- Je, ni lini Serikali itatekeleza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Old Korogwe kwenda Kwamndolwa - Magoma - Mashewa - Bombomtoni - Maramba hadi Mabokweni yenye urefu wa kilomita 127.54 kama ilivyoahidiwa na Mheshimiwa Rais pamoja na Waziri Mkuu kwa wananchi wa Korogwe?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru na nashukuru kwa majibu mazuri na Naibu Waziri, pia tunashukuru kwa ajili ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya matengenezo madogomadogo lakini matengenezo haya madogomadogo hayakidhi haja ya barabara hii kwani wakati wa mvua inaharibika kabisa na tunakosa mawasiliano kati ya mji mmoja hadi mwingine. Je, Serikali haioni kuna haja ya kutupa commitment ni wakati gani barabara hii itajengwa kwa kiwango cha lami ili tutatue changamoto hii kabisa? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE): Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Alfred James Kimea, Mbunge wa Korogwe Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ni kweli barabara zote za changarawe ama za udongo na hasa maeneo ya mwinuko inaponyesha mvua huwa zinakuwa na changamoto ya kuondoka udongo ama changarawe. Commitment ya Serikali pamoja kutekeleza ahadi ya Rais na Waziri Mkuu tayari Serikali inatafuta fedha ili tuweze kufanya usanifu wa kina ili barabara hii iweze kujengwa kwa kiwango cha lami. Kwa hiyo, Serikali inatafuta fedha na fedha ikipatikana barabara hii itajengwa kwa kiwango cha lami. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved