Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Florent Laurent Kyombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkenge

Primary Question

MHE. FLORENT L. KYOMBO Aliuliza:- (a) Je, ni kwa nini Jeshi la Wananchi wa Tanzania lisifuate utaratibu, ili kumiliki eneo la wananchi wa Kitongoji cha Byawamala, Kijiji cha Bulifani, katika Kata ya Kyaka, badala ya kuhamia eneo hilo kwa nguvu na hivyo kuibua mgogoro kuhusu eneo hilo? (b) Je, ni kwa nini eneo hilo lisigawanywe kwa Jeshi na Wananchi kwa kuwa eneo hilo ni kubwa na limekuwa pori kwa sasa?

Supplementary Question 1

MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Spika, nishukuru kwa nafasi ya swali la nyongeza, lakini niseme sijaridhika kabisa na majibu ya Serikali. Changamoto hii ipo tangu mwaka 78 ambapo sasa hivi ni takribani miaka 43 mpaka leo. Nilivyotumwa na wananchi wa Nkenge kuja kuleta malalamiko ya wananchi mwezi wa saba ndipo timu ikatumwa.

Mheshimiwa Spika, unaweza ukaona majibu ya Serikali. Anayelalamikiwa ni Wizara ya Ulinzi, ameenda yeye na JKT, hakuna kuhusisha Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, hakuna kuhusisha halmashauri, hakuna kuhusisha Mbunge aliyeleta malalamiko, hatuoni nia ya dhati ya kuweza kutatua tatizo hilo.

Mheshimiwa Spika, swali langu la msingi, kama ni kweli tunatambua kazi nzuri ya jeshi letu, Wizara ya Ulinzi kama ni kweli wanahitaji hilo eneo kuna utaratibu wa kuchukua eneo. Na swali langu la msingi lilikuwa ni hilo, kama linatakiwa kuchukuliwa na jeshi letu la ulinzi na usalama kwa nini wasifuate taratibu za Serikali ili eneo hilo basi lichukuliwe kwa mujibu wa taratibu? Hilo ni swali langu la kwanza.

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili. Anaposema kwamba, hilo eneo halitagawiwa kwa wananchi:-

Mheshimiwa Spika, siamini kama hiyo timu waliyounda ilienda site kwa sababu, wananchi wanaishi katika eneo hilo miaka 43 iliyopita. Sasa maana yake leo katika swali langu la pili atuambie hao wananchi walioko katika eneo hilo watapelekwa wapi? Nakushukuru.

Name

George Boniface Simbachawene

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibakwe

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri, lakini naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Florent Laurent Kyombo, Mbunge wa Nkenge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba, maeneo kama haya ambayo yanashika historia, lakini pia tunafahamu kwamba, eneo hili linalosemwa ndio lilitumika kama base dhidi ya Vita ya Kagera mwaka 78. Lakini tunafahamu pia madhara makubwa na madhila makubwa waliyoyapata watu wa Kagera na hususan wa maeneo haya. Maneno haya ya Mheshimiwa Mbunge na concern anayoiweka hapa inanifanya nitafakari zaidi na niombe kwa ruksa yako, acha tuchukue maoni yake na twende tukatafakari zaidi namna bora zaidi ya kutekeleza jambo hili kwa maslahi ya nchi, lakini kwa maslahi pia, ya watu wetu walioko katika eneo hili. Nakushukuru. (Makofi)