Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Amb. Adadi Mohamed Rajabu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muheza
Primary Question
MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB aliuliza:- Wakulima 1,128 wa msitu wa derema kata ya Amani Muheza wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu kupunjwa fidia ya mimea yao kutoka shilingi 3,315 kw a shina moja:- (a) Je, ni lini wakulima hapo watalipwa stahiki zao, (b) Je, kwa nini kwenye malip hayo Serikali sijijumiushe fidia ya ardhi yao?
Supplementary Question 1
MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza. Wakulima hawa wa Derema 1,128 wamekuwa na malalamiko ya muda mrefu na malalamiko yao hasa yanazingatia kwamba fedha ambazo wamelipwa fidia ni ndogo sana. Fedha hizo zimezingatia shina la mti wa iliki na shina la mti wa karafuu, halikuzingatia mazao ambayo yanatokana na yale mashina.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu, kwa kuzingatia ubinadamu, acha mbali hizo sheria: Je, Serikali iko tayari kuwaongezea wakulima hawa wa Derema fidia hiyo?
Pili, ni kweli kabisa kwamba wakulima hawa wanatakiwa kuhamishwa na unapomhamisha mtu inahitaji fedha nyingi sana. Wiki mbili zilizopita Waziri Lukuvi alikuwepo kwenye maeneo hayo ya Kibaranga, ametukabidhi hati ya shamba lililofutwa na Mheshimiwa Rais na tunategemea kuwahamisha watu hawa wa Derema kwenye shamba hilo la Kibaranga, lakini uwezo wa kujenga hawana. Mheshimiwa Naibu Waziri atakuwa tayari kuja kuongea na wananchi hawa wa Derema ili aweze kuwapa matumaini kwamba wataongezewa fidia yao kidogo?
Name
Eng. Ramo Matala Makani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduru Kaskazini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kuhusu swali la kwanza; kwanza, nampongeza kwa kuwaonea huruma wananchi wa Jimbo lake, lakini pia nampongeza kwa jitihada anazofanya kwa kuwatetea kila itakavyowezekana ili waweze kupata wanachostahili.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa ameshasema hata yeye mwenyewe kwamba majibu haya ni kwa mujibu wa sheria na utekelezaji wa ulipaji wa fidia pale awali ni kwa mujibu wa sheria na sasa anauliza kama Serikali inaweza kuangalia upande mwingine wa ubinadamu, nafikiri hoja ya msingi pale ni kuangalia kwamba fidia ambazo zinalipwa mahali pote, kwa nchi nzima kwa kweli, ziko kwenye viwango ambavyo vinatazamwa kuwa ni vya chini.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ubinadamu utatumika katika kwenda kuangalia upya sera na utatumika kwenda kuangalia upya sheria ili tuanzie kwenye ubinadamu lakini turekebishe sera zetu na sheria zetu kwa kuzingatia ubanadamu huo na ukweli na uhalisia ili malipo yaweze kulipwa kwa namna ambayo wananchi watakuwa wameona inakidhi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali la pili, nafikiri ni kama mwaliko kwamba niweze kupata nafasi ya kwenda, kwa sababu nikienda nitaona; na kuona ni kuamini. Basi namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, siyo tu mimi kwenda, nafikiri tuongozane naye twende tukaangalie, tuzungumze na wananchi hawa pengine tuwape elimu zaidi na kuweza kushirikiana nao katika kuona ukweli na kuweza kuona jambo gani linawezekana kufanyika kwa maslahi ya Taifa.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved