Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mohamed Lujuo Monni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chemba

Primary Question

MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza:- Je, ni lini Barabara ya Kwamtoro – Sanzawa – Mpendo yenye kilomita 58.2 itajengwa kwa kiwango cha kupitika msimu mzima kwani kwa sasa imekatika kutokana na mvua kubwa na kutojengwa kwa muda mrefu?

Supplementary Question 1

MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nasikitika sana swali langu halijajibiwa, swali limeuliza juu ya kilometa 58.2, nimejibiwa juu ya kilometa 23 tu. Naomba nirudi tena, ni lini Serikali itajenga barabara yote ya kilometa 58.2 kwa sababu sehemu kubwa ya barabara hiyo tayari imekatika kwa sababu ya mvua?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; barabara pia ya Larta – Lahoda – Handa imekatika kabisa hakuna namna watu wanaweza kupita. Naomba kupata majibu ya Serikali barabara hizi ni lini pia zitajengwa ili watu wapiti? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mohamed Monni, Mbunge wa Jimbo la Chemba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge ameuliza kwamba ni lini barabara inayopitia Lahoda na maeneo ambayo ameyaainisha kwamba itajengwa. Kama nilivyoeleza katika jibu la msingi kwamba katika mwaka huu wa fedha 2021/2022, TARURA kwa maana ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini umepanga kufanya tathmini ya barabara zote nchini pamoja na madaraja ili tuweze kuwa na database ya kutosha kuangalia zile barabara ambazo zinaharibika sana tuzipe kipaumbele katika mipango yetu inayokuja. Ndiyo maana nimeahidi kwamba moja ya barabara ambayo tutaipa kipaumbele ni hizi barabara ambazo ameitaja ikiwemo hii barabara ya Kwa Mtoro -Sanzawa – Mpendo ambayo tulikuwa tunaijenga kwa awamu kulingana na fedha inavyopatikana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge awe na Subira, Serikali ipo kazini na hatupo hapa kwa ajili ya kumdanganya mtu yeyote, lengo la Serikali ni kuwahudumia wananchi ili waweze kupata huduma bora kabisa ya usafiri na usafirishaji. Ahsante.