Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jafari Chege Wambura

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rorya

Primary Question

MHE. JAFARI W. CHEGE aliuliza:- Je, ni lini Bandari ya Sota eneo la Shirati itaanza kurekebishwa ili kuinua uchumi, lakini pia kuboresha shughuli za kibiashara eneo la mpakani mwa Tanzania na Kenya?

Supplementary Question 1

MHE. JAFARI W. CHEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nishukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri majibu ambayo yana matumaini. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, nje ya shughuli za kiuchumi na kibiashara ambazo wananchi wa Jimbo la Rorya watafaidika kutokana na urekebishwaji wa bandari hii, lakini pia ni pamoja na shughuli za kiusalama, hasa ukizingatia bandari hii iko mpakani kati ya nchi mbili.

Nilitaka nijue tu, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ni lini sasa bandari hii itaweza kutengewa fedha ili ianze kurekebishwa kama vile ambavyo swali la msingi limekuwa hasa ukizingatia bado hatujafanya hata ule upembuzi yakinifu kujua gharama za ujenzi wa bandari hii?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE): Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Jafari Chege Mbunge wa Rorya kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye jibu langu la msingi nilisema kuwa Bandari ya Sota ni kati ya bandari ambazo bado hazijawa rasmi lakini zimetambuliwa na Serikali ili ziweze kurasimishwa. Kwa hiyo isingekuwa rahisi kutenga fedha kupeleka kwenye bandari ambayo bado haijarasimishwa; na ndiyo maana tumesema kwaajili urasimishaji tathmini inafanyika ili hadi mwezi Agosti mwaka huu bandari hizo baada ya kuainishwa na kuona zina sifa zitarasimishwa na baada ya hapo fedha itatengwa kwa ajili ya kuzijenga ili ziweze kuwa rasmi ahsante.