Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jackson Gedion Kiswaga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalenga

Primary Question

MHE. JACKSON G. KISWAGA aliuliza: - Je, Serikali haioni uamuzi wa kutaka ifikapo tarehe 1 Mei, 2021 wasajili wa namba za simu za mkononi mitaani (freelancers) wawe katika maduka unaweza kufuta ajira zaidi ya 40,000 na kudhoofisha lengo lake la ajira milioni nane ifikapo mwaka 2025?

Supplementary Question 1

MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Waziri kwa majibu mazuri, pamoja na hayo nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza kwa kuwa asilimia 90 mpaka 95 ya wateja wapya kwenye mitandao ya simu wanapatikana kutokana na mfumo huu wa freelancer na Kampuni yetu ya TTCL imekuwa ikisuasua katika kuongeza wigo wake.

Je, lini sasa TTCL au Wizara itaagiza TTCL waweze kutumia mfumo huu ili waweze kuongeza wigo wao?

Swali langu la pili ni kwamba mfumo huu wa freelancer siyo ajira kamili, I mean vijana wamekuwa wakilipwa kwa njia ya commission na haya makampuni kwa mfano yana vijana kama laki moja hivi ambao wako kwenye mfumo huo. Sasa kutokana na kutokuwa na sheria inayotambua mfumo huu, hawa vijana wamekuwa wakitumia wakati mwingine loophole ya kuyashitaki haya makampuni kwamba wameajiriwa na hivyo kuleta hofu ya haya makampuni kuendelea kuajiri hawa vijana.

Je, Serikali italeta lini hapa sheria ili sasa itambue mfumo huu kwamba ni mfumo kamili ambao unasaidia kuajiri vijana wengi ambao hawana kazi? Ahsante sana.

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI MAWASILIANO TEKNOLOJIA NA HABARI:
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kiswaga Gedion Mbunge wa Kalanga kama ifuatavyo: -

Kwanza kabisa naomba nimpongeze Mbunge wa Kalenga Mheshimiwa Kiswaga kwa kazi kubwa anayoifanya kwa ajili ya Jimbo na wananchi wake wa Kalenga. Haya ni matakwa ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi kupitia ukurasa wetu wa 96, 97, 98 na ukurasa wa 113 kuongeza wigo wa mawasiliano kufikia asilimia 94. Sasa kupitia Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, tayari imeshatoa maelekezo kwa TTCL kuanza kutumia mfumo huu na mpaka sasa wana-agrigator watano na freelancer takribani 3000. Kwa hiyo, tutaendelea kuhakikisha kwamba tunasimamia hili ili waendelee kuongeza wigo mkubwa zaidi.

Mheshimiwa Spika, lakini suala la kamisheni kati ya freelancer na watoa huduma ni suala ambalo Serikali inaendelea kuhakikisha kwamba inaweka mfumo mzuri ambao utatumika katika kusimamia ili kuwepo na uwajibikaji kwa freelancer pamoja na watoa huduma ili kuhakikisha kwamba tunaondoa hili gap ambalo lilikuwa linasababisha na kutokana na uhalifu uliokuwa unatokea sababu ya freelancer kutumia hizi national ID kwa matakwa yao na si matakwa ambayo yamewekwa kisheria, ahsante.