Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Anne Kilango Malecela
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Same Mashariki
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO K.n.y. MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itatatua mgogoro uliopo katika eneo lenye madini ya Jasi kati ya Wananchi wa Kata ya Bendera Mkoani Kilimanjaro na Wananchi wa Kata ya Mkomazi Mkoani Tanga?
Supplementary Question 1
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kupata nafasi. Kwa sababu sehemu hizi mbili; Bendera na Mkomazi jambo kubwa wanalogombea ni mpaka kati ya Bendera na Mkomazi, ndiyo linapokuja suala la madini: Je, Serikali hamuoni ni muhimu sana Mkuu wa Mkoa akafika pale akaweka vizuri mpaka ule ili hili tatizo lililozungumzwa hapa ndani sasa hivi lisiendelee kutokea? Ahsante.
SPIKA: Haya tulikuwa na migogoro ya mipaka ya Wilaya kwa Wilaya, sasa huu mpaka wa Kata kwa Kata ambapo maana yake kuna vijiji na vijiji.
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Spika, ni mpaka wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mkoa wa Tanga, uko kati ya Bendera na Mkomazi.
SPIKA: Okay! Ni mipaka ya mikoa!
MHE. ANNE K. MALECELA: Ndiyo.
Name
William Vangimembe Lukuvi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ismani
Answer
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Anne Kilango Malecela. Kule kote ambako kuna migogoro ya tafsiri za mipaka sisi tunahusika. Kwa hiyo, hatutasita kwenda kutafsiri ardhini tafsiri ya mipaka iliyoainishwa na mwenye mamlaka. Tunazo GN, tutaifanya kazi hiyo. Nitaomba tu Mheshimiwa Kilango anipe maelezo ya ziada ili tuunde timu yetu ya pamoja ikafanye kazi hiyo. Hiyo ndiyo kazi yetu ya kutafsiri GN zilizoainisha mipaka na mwenye mamlaka. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved