Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ussi Salum Pondeza
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chumbuni
Primary Question
MHE. USSI SALUM PONDEZA aliuliza: - (a) Je, kwanini Serikali isihamishe Kambi za Jeshi la Wananchi (JWTZ) Zanzibar ambazo zipo katikati ya makazi ya watu kutokana na kasi ya maendeleo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza? na (b) Je, Serikali inachukua hatua gani za kumaliza mgogoro wa muda mrefu wa mpaka kati ya wakulima na JWTZ kambi ya Kisakasaka?
Supplementary Question 1
MHE. USSI SALUM PONDEZA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Ningependa nimuulize Mheshimiwa Waziri swali moja la nyongeza kama ifutavyo: -
Mheshimiwa Spika, amenijibu kuwa Serikali ina mpango wa kufanya upimaji na kufanya tathmini. Je, wakati itakapofika kufanya tathmini na upimaji, Mheshimiwa Waziri atakuwa tayari na mimi niambatane naye kwenda kwenye zoezi hilo? (Makofi/Kicheko)
Name
Dr. Stergomena Lawrence Tax
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nominated
Answer
WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Spika, ahsante, Mheshimiwa Mbunge ni mdau wetu na tutakuwa tayari kuongozana naye wakati zoezi hili likiendelea. (Makofi)
Name
Esther Nicholus Matiko
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. USSI SALUM PONDEZA aliuliza: - (a) Je, kwanini Serikali isihamishe Kambi za Jeshi la Wananchi (JWTZ) Zanzibar ambazo zipo katikati ya makazi ya watu kutokana na kasi ya maendeleo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza? na (b) Je, Serikali inachukua hatua gani za kumaliza mgogoro wa muda mrefu wa mpaka kati ya wakulima na JWTZ kambi ya Kisakasaka?
Supplementary Question 2
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru naomba kuuliza swali dogo la nyongeza. Wananchi wa Bugosi na Kenyambi kule Tarime Mjini walichukuliwa ardhi yao na Jeshi la Wananchi wa Tanzania tangu 2008, na jeshi hili au Serikali ilifanya tathmini mara ya kwanza 2013, 2017 wakafanya tathmini tena, 2019 na mara ya mwisho na ulitilia mkazo hapa Bungeni walikwenda kufanya uhakiki Juni, 2021 na wakatoa namba ya malipo na wakaahidi kwamba kufikia Agosti, 2021 watakuwa wamelipa lakini mpaka sasa hivi hawajawalipa wananchi hawa.
Mheshimiwa Spika, ningependa kujua ni lini sasa wananchi hawa wa Kenyambi na Bugosi watalipwa fidia zao, ili wapishe Jeshi la Wananchi wa Tanzania waende sehemu zingine kufanya makazi na shughuli za kimaendeleo?
Name
Dr. Stergomena Lawrence Tax
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nominated
Answer
WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Spika, naomba nimjibu Mheshimiwa Esther Matiko kama ifutavyo: -
Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema katika mkakati huo wa miaka mitatu tayari tumeshafanya tathmini na uhakiki katika maeneo yote isipokuwa maeneo ya Zanzibar ambayo ndiyo tutayafanyia quoter hii. Kinachoendelea sasa baada ya huu utathmini ni kufanya uhakiki na uhakiki unaendelea katika maeneo yote ambayo yamefanyiwa tathmini na uhakiki ili tukishakamilisha uhakiki taratibu nyingine zitafuata. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved