Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ally Anyigulile Jumbe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kyela
Primary Question
MHE. ALLY A. J. MLAGHILA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itahuisha Sera ya Maji ili iendane na wakati kwa kukidhi mahitaji halisi kwani kwa sasa haiendani na viwango vya kimataifa na imepitwa na wakati?
Supplementary Question 1
MHE. ALLY A. J. MLAGHILA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, nina maswali mawili ya nyongeza.
Kwa kuwa sera yetu sasa itachukua muda kuihuisha mpaka mwaka 2022; na kwa kuwa mpaka sasa kuna miradi mingi sana ya maji inaendelea na kwa kuwa pamoja na Sera hii kuna uhitaji wa maji wa kila mwananchi anahitaji kiasi gani kwa siku. Je, miradi inayofuata kwa sasa, Serikali imejipangaje kuhakikisha inakuwa endelevu?
Mheshimiwa Spika, la pili, mradi mmojawapo ambao umeathirika sana kwa Wilaya ya Kyela na hii Sera ya Maji ya watu 250 kuchota kwenye kituo kimoja ni Mradi wa Ngana group. Serikali imejipangaje sasa kuhakikisha mradi huu unafufuliwa na unakuwa katika viwango vya sasa ili kukidhi matarajio ya wana Kyela? Ahsante sana.
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili madogo ya nyongeza ya Mheshimiwa Ally Mlaghila, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwa miradi ambayo inaendelea sasa hivi ni miradi endelevu na tayari tunajitahidi kuhakikisha kuona kwamba tunapata vifaa vya kufanya uchunguzi kabla ya kuingia kwenye miradi na tumshukuru kabisa kwa kipekee Mheshimiwa Rais mama Samia Suluhu Hassan, kwa kupitia fedha ambazo tumepewa tayari tumeagiza mitambo saba kwa ajili ya kuchunguza maeneo ambayo yatatuletea vyanzo endelevu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa Mradi wa Ngana Group tayari umeshafufuliwa, wiki hii fedha zaidi ya shilingi milioni 500 tunaelekeza huko, ili kuona kwamba shughuli za awali zinaanza kutekelezwa. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved