Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Anastazia James Wambura

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA aliuliza: - (a) Je, ni lini Serikali itajenga air traffic control tower yenye urefu wa kutosha kumuwezesha muongoza ndege kuona miundombinu yote ya runway, taxiways na maegesho ya ndege katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara? (b) Je ni lini Serikali itajenga jengo la muda la abiria lenye ukubwa wa kutosha wingi wa abiria wanaoingia na kutoka katika uwanja huo? (c) Je, ni lini parking shade ya mitambo ya zimamoto na uokoaji itajengwa katika eneo lililopangwa kwenye master plan?

Supplementary Question 1

MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri na nampongeza sana kwa sababu aliweza hata kutembelea maeneo ya kiwanja hiki pamoja na mambo mengine aliyoweza kuyafanya. Nina maswali mawili ya nyongeza la kwanza kumekuwa na ongezeko la gharama za mradi awamu ya kwanza kwa kiasi cha takriban shilingi bilioni tano na ni kutokana na sababu mbalimbali na moja ya sababu ni kuchelewa kukamilika kwa mradi huu awamu ya kwanza.

Mheshimiwa Spika, lakini kwa hesabu za haraka haraka hizi bilioni tano zingeweza hata kujenga vituo takriban 10 vya afya. Swali langu je, nini kauli ya Serikali kuhusiana na ongezeko hili la shilingi bilioni tano?

Mheshimiwa Spika, Swali la pili kama alivyoeleza Mheshimiwa Waziri, ni kwamba maboresho ya uwanja huu yamelenga kukidhi ongezeko kubwa la shughuli za kiuchumi na kijamii katika mikoa ya Kusini. Na ili kupandisha daraja kutoka Code 3c hadi 4e ni lazima ujenzi wa awamu ya pili ukamilike. Swali langu ni kwamba je ni lini awamu ya pili ya mradi huu itaanza? Ahsante.

Name

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkoani

Answer

WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali ya nyongeza mawili ya Mheshimiwa Wambura kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kumekuwa na ongezeko la shilingi bilioni tano kwenye ujenzi huu na sababu kubwa iliyosababisha kuongezeka kwa bei hiyo, ni kutokana na makisio halisi hasa ya kufunga taa mwanzo ilikisiwa ni shilingi bilioni 2.2 lakini baada ya kupata mkandarasi gharama ikaenda mpaka bilioni 6 pia na kwenye fire equipment (gari la kuzimia moto) makisio yalikuwa milioni 800 na ilikwenda mpaka bilioni 1.5 kwa vile hii ndiyo iliyosababisha ongezeko liongezeke mpaka kwa shilingi bilioni tano.

Mheshimiwa Spika, swali la pili ni lini uwanja huu tutaweza kufungwa hizo taa. Awamu ya pili ambayo ni kufunga taa pamoja na kujenga jengo la control tower pamoja na jengo la abiria utaanza mara moja tu mara itapomalizika awamu ya kwanza ambayo itakuwa kunako mwezi Julai mwaka huu.

Name

Issa Ally Mchungahela

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lulindi

Primary Question

MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA aliuliza: - (a) Je, ni lini Serikali itajenga air traffic control tower yenye urefu wa kutosha kumuwezesha muongoza ndege kuona miundombinu yote ya runway, taxiways na maegesho ya ndege katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara? (b) Je ni lini Serikali itajenga jengo la muda la abiria lenye ukubwa wa kutosha wingi wa abiria wanaoingia na kutoka katika uwanja huo? (c) Je, ni lini parking shade ya mitambo ya zimamoto na uokoaji itajengwa katika eneo lililopangwa kwenye master plan?

Supplementary Question 2

MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona lakini kumekuwa na ucheleweshaji wa mara kwa mara wa kusaini document za kuendeleza mradi. Je, Serikali inachukua hatua gani za kuharakisha mradi huu kusudi uende sambamba na maendeleo ya mradi wa bandari.

Name

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkoani

Answer

WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kumjibu Mheshimiwa Mbunge swali lake la nyongeza kama ifuatavyo. Nia ya Serikali si kuchelewesha mradi Serikali siku zote tunataka mradi uanze mara moja lakini kuna matatizo ambayo baadhi ya wakati hayawezi kuepukika. Kwa mfano sasa hivi kulikuwa na shida ya ugonjwa wa corona na vifaa vingi hasa vile vya taa vilikuwa vinatoka nje kwa vile hiyo ilisababisha mradi uweze kuchelewa kidogo.

Name

Jacqueline Kandidus Ngonyani (Msongozi)

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA aliuliza: - (a) Je, ni lini Serikali itajenga air traffic control tower yenye urefu wa kutosha kumuwezesha muongoza ndege kuona miundombinu yote ya runway, taxiways na maegesho ya ndege katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara? (b) Je ni lini Serikali itajenga jengo la muda la abiria lenye ukubwa wa kutosha wingi wa abiria wanaoingia na kutoka katika uwanja huo? (c) Je, ni lini parking shade ya mitambo ya zimamoto na uokoaji itajengwa katika eneo lililopangwa kwenye master plan?

Supplementary Question 3

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kuniona nipende kuuliza swali la nyongeza kama ifuatavyo. Barabara ya Likuyufusi Mkenda ina urefu wa kilometa 124 na ni barabara ya kimkakati inayounganisha Mkoa wa Ruvuma na nchi yetu ya Mozambique.

Je, ni lini Serikali itaanza kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami?

Name

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkoani

Answer

WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, naomba kumjibu Mheshimiwa Ngonyani kama ifuatavyo. Ni kweli barabara hii Mheshimiwa Jenista amekuwa akiuliza muda mrefu ni barabara muhimu tunaijua na ina maendeleo makubwa kwa ajilii ya wananchi wa kule kwa vile Mheshimiwa Ngonyani naomba nikwambie kwamba hii barabara tunaitambua vizuri na iko kwenye mpango wa Serikali na sasa tuko kwenye hatua za mwisho za kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo.

Name

Abdallah Dadi Chikota

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyamba

Primary Question

MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA aliuliza: - (a) Je, ni lini Serikali itajenga air traffic control tower yenye urefu wa kutosha kumuwezesha muongoza ndege kuona miundombinu yote ya runway, taxiways na maegesho ya ndege katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara? (b) Je ni lini Serikali itajenga jengo la muda la abiria lenye ukubwa wa kutosha wingi wa abiria wanaoingia na kutoka katika uwanja huo? (c) Je, ni lini parking shade ya mitambo ya zimamoto na uokoaji itajengwa katika eneo lililopangwa kwenye master plan?

Supplementary Question 4

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi changamoto ya uwanja wa ndege wa Mtwara ni pamoja na gari ya zimamoto na kwa kuwa fedha za ununuzi wa gari ya zimamoto ipo kwenye hatua ya mwanzo ya ukarabati ya uwanja.

Je, Serikali itakamilisha lini mchakato wa ununuzi wa gari hili jipya la zimamoto?

Name

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkoani

Answer

WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Abdallah kama ifuatavyo. Kama nilivyosema katika vitu ambavyo tunataka kufanya ni ununuzi wa gari la zimamoto ambalo tumetenga shilingi bilioni 1.5 na hivi sasa tayari tumeshampata mkandarasi kwa ajili ya kuleta gari hilo.